Thursday, April 11, 2013

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein Azindua Mradi wa Umeme wa Njia ya Pili ,Kutoka Ubungo Jijini Dar es Salaam Mpaka Mtoni Mjini Zanzibar.







Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la ‘Millennium Challenge’ MCC,Daniel Yohannes Ceo, akitoa hutuba yake kwa Wananchi wa Zanzibar wakati wa Sherehe za uzinduzi wa Mradi wa Umeme wa Njia ya Pili kutoka Ubungo Dar es Salaam mpaka Mtoni,uliofadhiliwa na Shirika la Misaada la MCC la Marekani,sherehe hizo zilifanyika katika uwanja wa Amaan mjini Unguja.


Balozi wa Marekeni nchini Tanzania Alfonso Lenhardt,akitoa hutuba yake kwa Wananchi wa Zanzibar wakati wa Sherehe za uzinduzi wa Mradi wa Umeme wa Njia ya Pili kutoka Ubungo Dar es Salaam mpaka Mtoni,uliofadhiliwa na Shirika la Misaada la MCC la Marekani,sherehe hizo zilifanyika katika uwanja wa Amaan mjini Unguja
Hiki ni Kituo kikuu cha Umeme cha Mtoni Unguja.ambacho tayari Mradi wake uliofadhiliwa na MCC Marekani umezinduliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,kwa pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la ‘Millennium Challenge’ MCC,Daniel Yohannes Ceo, pia Balozi wa Marekani Nchini Tanzania ALfonso Lenhardt, alihudhuria katika uzinduzi huo,utakaochukua Ukubwa wa Kilowati 100.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akikata utepe na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la ‘Millennium Challenge’ MCC,Daniel Yohannes Ceo, kama ishara ya uzinduzi mradi wa Umeme wa Njia ya Pili ,kutoka Ubungo Dar es Salaam mpaka Mtoni,ukiwa umefadhiliwa na Shirika la Misaada la MCC la Marekani,hafla hiyo ilifanyika jana katika kituo kikuu cha Umeme Mtoni Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akifungua pazia kuzindua mradi wa Njia ya Pili ya Umeme,kutoka Ubungo Dar es Salaam mpaka Mtoni,ukiwa umefadhiliwa na Shirika la Misaada la MCC la Marekani,hafla hiyo ilifanyika jana katika kituo kikuu cha Umeme Mtoni Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la ‘Millennium Challenge’ MCC,Daniel Yohannes Ceo,(katikati) na Balozi wa Marekani Nchini Tanzania ALfonso Lenhardt,wakipata maelezo ya kiutendaji kazi katika kituo kikuu cha umeme kutoka Ubungo Dar es Salaam mpaka Mtoni,ukiwa umefadhiliwa na Shirika la Misaada la MCC la Marekani,kwa Meneja wa Shirika la Umeme Zanzibar Hassan Ali,(kushoto) baada ya ufunguzi rasmi jana.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,(katikati) na wageni wake Balozi wa Marekeni nchini Tanzania Alfonso Lenhardt,na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la ‘Millennium Challenge’ MCC,Daniel Yohannes Ceo,pamoja na Viongozi wengine wakiangalia majarida yaliyocha pishwa kuhusu mradi huo wa Umeme wakati wa Sherehe zilizofanyika uwanja wa Amaan Studium,

Baadhi ya Wananchi wa Manispaa ya Mji wa Unguja, wakiwa katika sherehe maalum za Uzinduzi wa Mradi wa Umeme wa Njia ya Pili kutoka Ubungo Dar es Salaam mpaka Mtoni,uliofadhiliwa na Shirika la Misaada la MCC la Marekani,na akiwa Mgeni Rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,

Baadhi ya Wananchi wa Manispaa ya Mji wa Unguja, wakiwa katika sherehe maalum za Uzinduzi wa Mradi wa Umeme wa Njia ya Pili kutoka Ubungo Dar es Salaam mpaka Mtoni,uliofadhiliwa na Shirika la Misaada la MCC la Marekani,na akiwa Mgeni Rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.-Zanzibar

Tags:

0 Responses to “Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein Azindua Mradi wa Umeme wa Njia ya Pili ,Kutoka Ubungo Jijini Dar es Salaam Mpaka Mtoni Mjini Zanzibar. ”

Post a Comment

Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.

HHHHHHHHHHHH

Subscribe

Kwa habari na Taarifa weka Email yako Hapa tutakutumia

© 2014 FUNUNU HABARI.. All rights reserved.
Designed by FUNUNU HABARI