Tuesday, April 9, 2013

MWAKYEMBE ASHANGAZWA NA ONGEZEKO KUBWA LA NAULI NA..AMETOA AMRI NAULI ZA TRENI ZISIPANDE




Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe amewatuliza Watanzania kuhusu kupanda kwa nauli akisema ameyapokea malalamiko yao na atayafanyia kazi. 


Kwa kuanzia ameagiza nauli za treni jijini Dar es Salaam zisipande bali ziendelee kutozwa za zamani mpaka taarifa zaidi itakapotolewa.

Mwakyembe alitoa kauli hiyo alipozungumza kwenye Bonanza la Vyombo vya Habari lililofanyika jijini Dar es Salaam jana.

Alisema ni kweli Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra|) ilitangaza nauli mpya, lakini kwa kilio cha Watanzania ataangalia sababu za kupandisha huku akishirikiana na wasafirishaji kujua ukweli.

Tags:

0 Responses to “MWAKYEMBE ASHANGAZWA NA ONGEZEKO KUBWA LA NAULI NA..AMETOA AMRI NAULI ZA TRENI ZISIPANDE”

Post a Comment

Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.

HHHHHHHHHHHH

Subscribe

Kwa habari na Taarifa weka Email yako Hapa tutakutumia

© 2014 FUNUNU HABARI.. All rights reserved.
Designed by FUNUNU HABARI