Tuesday, April 9, 2013
SUPER SPORT YAPANGUA MECHI ZA SIMBA NA YANGA
Tuesday, April 9, 2013 by Unknown
Nembo ya kituo cha luninga Super Sports
MECHI sita za Ligi Kuu Bara zimesogezwa mbele ili zionyeshwe moja kwa moja na kituo cha televisheni cha Super Sports cha Afrika Kusini.
Mechi hizo ambazo zimepewa jina la Super Week zitachezwa kati ya Aprili 11 na Mei 18.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Bonifance Wambura alizijata mechi ambazo zitarushwa laivu kuwa zile zilizokuwa zichezwe Aprili 10, lakini sasa zitachezwa Aprili 11 ambazo ni Azam dhidi ya African Lyon kwenye Uwanja wa Chamazi na Yanga na Oljoro JKT Aprili 13 badala ya Aprili 10 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Simba na Azam watacheza Aprili 14 kwenye Uwanja wa Taifa wakati Coastal Union na JKT Ruvu ni Aprili 16.
Mechi nyingine ya Super Week itakayochezwa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga ni kati ya Mgambo Shooting na Yanga, Aprili 17. Mechi nyingine ya laivu ni Yanga na Simba itakayochezwa Mei 18 jijini Dar es Salaam.
Kutokana na mechi za Super Week, mechi kati ya Mtibwa Sugar na Oljoro JKT iliyokuwa ichezwe Aprili 13 sasa itachezwa Aprili 17, Manungu, Turiani mkoani Morogoro.
Tags:
burudani ,
michezo
This post was written by: Author Name
Author description goes here. Author description goes here. Follow him on Twitter
Get Updates
Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.
Related Articles
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “SUPER SPORT YAPANGUA MECHI ZA SIMBA NA YANGA”
Post a Comment
Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.