Friday, April 5, 2013

"NATONGOZWA SANA FACEBOOK JAMANI"...CHUCHU HANS






Msanii wa filamu Bongo ambaye ni mke wa mtu, Chuchu Hans amefunguka kuwa anatongozwa sana na wanaume kupitia Mtandao wa Kijamii wa Facebook, kitendo kinachomkosesha amani.

Akizungumza na mwandishi wetu, Chuchu alisema kuwa, anachojua yeye mtandao huo ni sehemu ya kukutana na marafiki na kubadilisha mawazo lakini cha ajabu kila akiingia, wanaume kibao wamekuwa wakimtaka.

“Mimi kwa kweli kila nikiingia Facebook nakutana na wanaume ambao wananitongoza, mtu anajua kabisa una mtu wako lakini bila haya anatangaza dau na kueleza kuwa, anakutaka, mijitu hii naichukia kweli,” alisema Chuchu

Tags: ,

0 Responses to “"NATONGOZWA SANA FACEBOOK JAMANI"...CHUCHU HANS ”

Post a Comment

Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.

HHHHHHHHHHHH

Subscribe

Kwa habari na Taarifa weka Email yako Hapa tutakutumia

© 2014 FUNUNU HABARI.. All rights reserved.
Designed by FUNUNU HABARI