Wednesday, April 10, 2013

Shilole Anaswa Akijivinjari na Bwana wa Kidhungu..


SIKU chache baada ya kuripotiwa akijiachia kimalavidavi na ‘lejendari’ wa Bongo Fleva, Aboubakar Katwila, staa wa muziki na filamu za Kibongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amenaswa hotelini na bwana Mzungu aliyetajwa kwa jina moja la George, kamera za Risasi Mchanganyiko ni noma.

Kwa mujibu wa shushushu wetu, tukio hilo lilijiri hivi karibuni katika hoteli moja maarufu jijini hapa ambapo Shilole alikuwa kwenye ziara ya shoo yake.
Ilidaiwa kuwa mara tu baada ya kumaliza ziara ya shoo, Shilole hakuondoka jijini hapa na badala yake alionekana sehemu tofauti akijivinjari na jamaa huyo ambaye uchunguzi wetu ulibaini kuwa ni bosi wa klabu moja maarufu ya usiku Kanda ya Ziwa.

Kabla ya kuondoka katika jiji hili la sangara na sato, Alhamisi iliyopita na ndege ya jioni, Shilole alinaswa kimalavidavi na Mtasha huyo Jumatano katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere wa Gold Crest kulipokuwa na maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Syria.
Shilole alishuhudiwa akifanyiwa ‘shopping’ ya kufuru na bwana huyo ambapo gazeti hili lilinasa mpango mzima ambapo lilipotaka kujua kama ni wapenzi, Mtasha huyo alijibu kwa kifupi sana: “No comment” (sina la kusema).

Kwa upande wake Shilole alipobanwa mbavu alifunguka: “Nisingependa kuongelea jambo hilo kwani sasa najipanga kimuziki zaidi, shopping ni mambo ya kawaida sana kwa hiyo ni vyema tukaongelea muziki wangu kwani shoo yangu ya Pasaka ilijaa mashabiki wa kufa mtu so nakubalika sana Mwanza na siku moja nitaweka makazi hapa.”

Tags: ,

0 Responses to “Shilole Anaswa Akijivinjari na Bwana wa Kidhungu..”

Post a Comment

Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.

HHHHHHHHHHHH

Subscribe

Kwa habari na Taarifa weka Email yako Hapa tutakutumia

© 2014 FUNUNU HABARI.. All rights reserved.
Designed by FUNUNU HABARI