Saturday, May 4, 2013

Bocco aikosesha Azam ushindi,akosa penalti muhimu


Kipa wa AS FAr Rabat, Ali Grouni akimfariji mshambuliaji wa Azam FC, John Bocco baada ya kukosa penalti ambayo ingeipa Azam tiketi ya kufuzu Kombe la Shiriksiho jioni hii kwenye Uwanja wa Prince Moulay Abdellah, Rabat. Azam imefungwa 2-1.               Mahmoud Zubeiry, Rabat
SOKA ni mchezo wa bahati wakati mwingine. Naam sadakta, usemi huo umedhihirika leo kwenye Uwanja wa Prince Moulay Abdellah baada ya Azam kulala 2-1 mbele ya wenyeji AS FAR Rabat na kutolewa katika Raundi ya Tatu ya Kombe la Shirikisho Afrika, licha ya kupata nafasi nzuri ya kusonga mbele dakika ya 81.
“Tumekosa penalti dakika ya 81, siwezi kumlaumu refa ikiwa tumekosa penalti zimebaki dakika tisa,” alisema kocha wa Azam FC, Muingereza Stewart Hall baada ya mchezo akizungumza na BIN ZUBEIRY.
Azam ilihitaji sare yoyote ya mabao ifuzu na ilikaribia kuipata dakika ya 81 ilipopata penalti ikiwa nyuma kwa mabao 2-1, lakini fundi wa upigaji wa michomo hiyo, John Raphael Bocco alikwenda kugongesha mwamba mpira huo.
Dakika ya 88, kona nzuri iliyochongwa na Khamis Mcha ‘Vialli’ iliunganishwa vizuri kwa kichwa na Bocco, lakini beki mmoja wa Rabat akaiwahi kwenye chaki na kuiondosha kwenye eneo la hatari. Katika mechi hiyo iliyochezeshwa na refa Abib Charef Medh aliyesaidiwa na Mahmoud Bitam na Mohamed Mekous wote kutoka Algeria, hadi mapumziko, Rabat walikuwa mbele kwa mabao 2-1.
Azam ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao dakika ya sita, mfungaji John Raphael Bocco kwa mpira wa adhabu, baada ya beki mmoja wa Rabat kuunawa mpira kwenye eneo la hatari. Boko alipiga shuti zuri ambalo liliupita ukuta wa Rabat na kumpoteza maboya kipa wao, Ali Grouni na kutinga nyavuni. Mashabiki wa Rabat walianzisha fujo baada ya bao hilo na kujikuta wakipambana na Polisi. Idadi ya Polisi iliongezwa uwanjani ili kuwadhibiti mashabiki hao ambao walikuwa wakivunja viti na kuwatupia Polisi.  Iliwachukua dakika sita tu Rabat kusawazisha kupitia kwa Abdelrahim Achchakir kwa mkwaju wa penalti, baada ya beki David Mwantika kumchezea rafu mchezaji wa Rabat.a

Tags:

0 Responses to “Bocco aikosesha Azam ushindi,akosa penalti muhimu ”

Post a Comment

Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.

HHHHHHHHHHHH

Subscribe

Kwa habari na Taarifa weka Email yako Hapa tutakutumia

© 2014 FUNUNU HABARI.. All rights reserved.
Designed by FUNUNU HABARI