Saturday, May 4, 2013
Penzi la Wema lamtesa Prezo,akwepa swali
Saturday, May 4, 2013 by Unknown
Dar es Salaam, Tanzania
BAADA ya uvumi kwamba msanii wa muziki wa kizazi kipya wa Kenya Prezo kuzama kwenye mahaba mazito na msanii wa filamu nchini Tanzania Wema Sepetu, Msanii huyo ameshikwa na kigugumizi na kushindwa kukanusha tuhuma hizo.
Prezo ambaye alifiwa na mchumba wake ambaye pia alikuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Nigeria marehemu Goldie Harvey, aliyefariki dunia February mwaka huu, juzi alishindwa kudhibitisha tuhuma hizo baada ya kuulizwa swali na kushindwa kulijibu.
Prezo ambaye yuko nchini kwa ziara ya muziki alionekana katika picha za mahaba akiwa na Wema Sepetu, hata hivyo Wema aliwahi kukanusha picha hizo na kudai kwamba walipiga wakati walipokuwa wakirekodi filamu mpya ya Wema na kwamba hana mahusiano yoyote ya mapenzi na msanii huyo.
Akiwa katika mahojiano maalum kwenye kipindi cha mapenzi kilichorushwa usiku na Redio Clouds FM Prezo alishikwa na kwi kwi cha gafla baada ya kutakiwa kudhibitisha juu ya uvumi kwamba amenasa kwenye mahaba mazito na mrembo huyo mwenye skendo za kubadilisha wanaume kila kukicha.
Mtangazaji wa kipindi hicho, Loveness maarufu kwa jina la Diva alimtaka Prezo kuweka bayana juu tuhuma hizo, hata hivyo Prezo alishindwa badala yake akaanza kujing'ata ng'ata huku akipotezea swali hilo kwa kuingiza bada nyingine.
"Prezo twambie kuhusu mahusiano yako wewe na Wema Sepetu, kuna uvumi kwamba umezama kwenye mapenzi yake je hili lina ukweli gani?" aliuza Diva, hata hivyo baada ya swali hilo Prezo alitoka nje ya swali na kuzungumzia masuala mengine kwa lengo la kukwepa kutoa jibu, hata alipoulizwa tena kwa mara ya pili na yatatu, Prezo akasema bado unaulizwa swali hilo hepu tuliache.
Kitendo cha Prezo kushindwa kujibu swali hilo ni ishara kwamba wawili hao wameanza kuimarisha mahusiano yao na kwamba wasinge penda kulizungumzia kwani bado ni mapema sana.
Tags:
mapenzi
This post was written by: Author Name
Author description goes here. Author description goes here. Follow him on Twitter
Get Updates
Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.
Related Articles
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “Penzi la Wema lamtesa Prezo,akwepa swali ”
Post a Comment
Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.