Home
» kitaifa
» UPDATE: RAIS KIKWETE AKATIZA ZIARA YAKE NCHINI KUWAIT.....ANARUDI NCHINI KUJUMUIKA NA WAHANGA WA BOMU LA JANA
Monday, May 6, 2013
UPDATE: RAIS KIKWETE AKATIZA ZIARA YAKE NCHINI KUWAIT.....ANARUDI NCHINI KUJUMUIKA NA WAHANGA WA BOMU LA JANA
Monday, May 6, 2013 by Unknown
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumatatu, Mei 6, 2013, ameamua kukatiza ziara yake ya Kiserikali nchini Kuwait ili kurejea nyumbani kutokana na tukio la shambulio la kigaidi la mlipuko mjini Arusha ambako watu wawili wamefariki na 60 wamejeruhiwa.
Rais Kikwete alikuwa aondoke kesho kurejea nyumbani, amekatiza ziara hiyo na anaondoka Kuwait City kurejea nyumbani mara moja ili kuwa karibu na wafiwa pamoja na wale waliojeruhiwa katika shambulio hilo la kigaidi.
Miongoni mwa shughuli ambazo hazitafanyika sasa kutokana na uamuzi huo wa Rais ni ziara ya kutembelea Kampuni ya Mafuta ya Kuwait katika eneo la Ahmadi mjini Kuwait.
Aidha, Rais hatahudhuria dhifa ya chakula cha jioni ambacho alikuwa anaandaliwa na Waziri Mkuu wa Kuwait, Mheshimiwa Sheikh Jaber Al Mubarak Al Hamad Al Sabah.
Tags:
kitaifa

This post was written by: Author Name
Author description goes here. Author description goes here. Follow him on Twitter
Get Updates
Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.
Related Articles
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

0 Responses to “UPDATE: RAIS KIKWETE AKATIZA ZIARA YAKE NCHINI KUWAIT.....ANARUDI NCHINI KUJUMUIKA NA WAHANGA WA BOMU LA JANA ”
Post a Comment
Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.