Tuesday, June 11, 2013

Fabregas Azikata Maini Arsenal Na Man United: Siondoki Barcelona Ng’oo Labda Walazimishe Kuniuza


CESC FABREGAS amesisitiza kuwa ataondoka Barcelona iwapo tu watamchoka na kulazimisha kumuuza.

Fabregas ambaye alijunga na Barcelona kwa pauni milioni 40 kutoka Arsenal mwaka 2011, amekuwa akihusishwa kurejea Ligi kuu ya Uingereza, huku kipaumbele kikiwekwa zaidi kwa Arsenal ingawa Manchester United nao wamo.

Lakini Fabregas amesema: “Imenichukua muda mrefu kufika hapa nilipo, na sitegemei kuitupa nafasi hii kirahisi.

“Kama Barcelona watasema hawanihitaji hilo litakuwa ni jambo lingine – lakini shida yangu ni kubakia Barca.

“Imekuwa ni njozi yangu tangu utotoni. Barcelona ni nyumbani kwangu na siku zote nimekuwa nikiota kushinda mataji hapa.”

Fabregas alikosolewa na mashabiki wa Barcelona katika msimu wake wa kwanza kurejea nyumbani.

Alisema: “Baadhi ya watu wanaweza wakawa hawavutiwi na uchezaji wangu lakini linanipa changomoto ya kujituma zaidi.

“Kama mashabiki wananizomea, nahitaji kulipokea hilo. Nilikuwa mtu wa kwanza kujua kuwa hii itakuwa changamoto kubwa katika maisha yangu. Nataka kucheza.”



Tags:

0 Responses to “Fabregas Azikata Maini Arsenal Na Man United: Siondoki Barcelona Ng’oo Labda Walazimishe Kuniuza”

Post a Comment

Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.

HHHHHHHHHHHH

Subscribe

Kwa habari na Taarifa weka Email yako Hapa tutakutumia

© 2014 FUNUNU HABARI.. All rights reserved.
Designed by FUNUNU HABARI