Home
» michezo
» MAANDALIZI YA MTANANGE WA KUKATA NA SHOKA KATI YA TIMU YA NMB NA WABUNGE UWANJA WA JAMHURI
Wednesday, June 12, 2013
MAANDALIZI YA MTANANGE WA KUKATA NA SHOKA KATI YA TIMU YA NMB NA WABUNGE UWANJA WA JAMHURI
Wednesday, June 12, 2013 by Unknown
Timu ya Benki ya NMB ipo kwenye maandalizi makubwa ya mechi kati
yao na wabunge ambayo itachezwa siku ya jumamosi kwenye viwanja vya
Jamhuri hapa Dodoma. Ili kufanikisha mtanange huo Benki ya NMB
imekabidhi jezi kwa Nahodha wa timu ya Bunge ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) Kassim Majaliwa. Ni mtanange wa kukata na shoka ambao
umesubiriwa kwa hamu na kwa muda mrefu na mashabiki wa timu hizo mbili.
Mheshimiwa Kassim Majaliwa akipokea jezi kwa ajili ya mechi hiyo kati ya Wabunge na NMB kutoka kwa Nahodha msaidizi wa timu ya NMB, Hezbon Mpate. Makabidhiano haya ya Jezi zenye thamani ya shilingi milioni tatu na laki saba yamefanyika katika viwanja vya bunge jijini Dodoma.
Mheshimiwa Fatma Mikidadi akipokea jezi za mpira wa pete kutoka
kwa nahodha wa timu ya mpira wa pete ya NMB Josephine Kulwa. Mechi zote
zinatarajiwa kuchezwa siku ya jumamosi katika viwanja vya Jamhuri mjini Dodoma.
Waheshimiwa wabunge pamoja na maofisa wa NMB wakizifurahia jezi mara baada ya makabidhiano rasmi.

This post was written by: Author Name
Author description goes here. Author description goes here. Follow him on Twitter
Get Updates
Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.
Related Articles
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MAANDALIZI YA MTANANGE WA KUKATA NA SHOKA KATI YA TIMU YA NMB NA WABUNGE UWANJA WA JAMHURI ”
Post a Comment
Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.