Home
» siasa
» Picha : Baaadhi ya Picha za Matukio Bomu lilolipuka Baada ya Mkutano Wa Chadema Kaloleni Arusha leo.
Saturday, June 15, 2013
Picha : Baaadhi ya Picha za Matukio Bomu lilolipuka Baada ya Mkutano Wa Chadema Kaloleni Arusha leo.
Saturday, June 15, 2013 by Unknown

HAWA NDIYO WALISHAMBULIWA KWA BOMU NA KUOFIWA KUFA
BAADHI YA MAJERUHI WA BOMU LAKUTUPWA KWENYE MKUTANO WA CHADEMA SOWETO
HIZI NI DAMU ZILIZOTAPAKA HAPA CHINI
HIZI NI DAMU ZILIZOTAPAKA HAPA CHINI
HIZI NI DAMU ZILIZOTAPAKA HAPA CHINI
BAADA YA BOMU KAMANDA MBOWE AKIFANYA JUHUDI ZA KUWATAFUTIA USAFIRI MAJERUHI
WANANCHI WAKIWA WAMEPIGWA NA MSHANGAO BAADA YA BOMU KULIPUKA
BAADA YA BOMU KAMANDA MBOWE AKIFANYA JUHUDI ZA KUWATAFUTIA USAFIRI MAJERUHI
BAADA YA BOMU KAMANDA MBOWE AKIFANYA JUHUDI ZA KUWATAFUTIA USAFIRI MAJERUHI
LEMA AKIWA NA MBOWE WANAJADILIANA BAADA YA BOMU KULIPULIWA
MWESHIMIWA MBOWE AKIKIMBIA BAADA YA POLISI KUANZA KUPIGA MABOMU YA MACHOZI
PICHANI NI BOMU LA MACHOZI LILILORUSHWA NA POLISI BAADA YA TUKIO LA BOMU
AWALI KABLA YA TUKIO HILO MAKAMANDA WAKIWA JUKWAANI
LEMA AKIONGE NA WANANCHI
WATU WAKIWA WAMEACHA NJIA HILI KAMANDA APITE
KAMANDA MBOWE AKIWA ANAINGIA
Uwanja wa Soweto ambapo Mkutano wa Chadema kufunga kampeni za kuwania Udiwani Kata ya Kaloleni Jijini Arusha ulikuwa unafanyika umegeuka kuwa uwanja wa vilio baada ya kinachodhaniwa kuwa bomu kulipuka na kuua watu watatu na zaidi ya 50 kujeruhiwa vibaya huku baadhi yao wakiwa wamevunjika miguu.
Katika Mkutano huo walikuwapo pia Mwenyekiti wa Chadema naa Mbunge wa Arusha Mjini, Mh Godbless Lema sambamba na viongozi wengine wa Chadema Mkoa wa Arusha lakini bahati nzuri Mbowe na Lema ambao walokuwa vinara katika Mkutano huo hawakudhurika moja kwa moja na mlipuko huo.
Mlipuko huo ulitokea mbele ya gari ambalo lilikuwa ni jukwaa la matangazo mara baada tu ya Mh Mbowe, Lema na viongozi wote waliokuwa jukwaa kuu kushuka chini na kujichanganya katikati ya watu wakikusanya michango ya watu, hali inayoashiria mrushaji huenda lilenga kuwajeruhi viongozi hao.
Miili ya marehemu na majeruhi walipelekwa hospitali ya Mt Meru lakini hawakupokelewa baada ya kilichoelezwa ni vurumai iliiyoletwa na mamia ya wafuasi wa Chadema waliokuwa na hasira baada ya wenzao kuuwawa.
Baadhi ya majeruhi ni viongozi wa Chadema ngazi ya Kata, Wilaya na Mkoa wa Arusha, sambamba na wananchi wa kawaida wakiwemo watoto waliofika mkutanoni hapo.
Mkutano wa leo ulivunja rekodi ya mahudhurio viwanjani hapo.. lakini ulikuja kuharibika baada ya kutokea mlipuko huo haotuba zikiwa zimeishamalizika na baadhi ya watu wakiwa wanatawanyika kuelekea majumbani huku zoezi la kuchangisha pesa likiendelea, kitendo kilichowazuia hata wakusanyaji michango kushindwa kumalizia zoezi hilo…
Hali ikiwa bado tete viwanjani hapo, magari kadhaa ya askari polisi yalifika huku askari wakiwa na silaha lakini walilazimika kupiga mabomu ya machozi kadhaa hewani na kisha kuondoka kutokana na baadhi ya wananchi waliokuwa na hasira kuwafuata na kupaza sauti wakitaka wawaue pia.
Kijana mmoja muuza machungwa aliieleza blogu hii kuwa aliyerusha bomu hilo alitokea upande wa nyuma ya jukwaa kuu na badae kukimbilia nyumba zilizojirani.
Mwenyekiti wa Chadema, Mh Freeman Mbowe akiwasili viwanja vya Soweto, Kata ya Kaloleni Jijini Arusha jioni ya leo katika Mkutano wa Chadema kufunga kampeni zake.
Mh Mbowe akichangisha pesa mkutanoni hapo sekunde chache kabla ya mlipuko kutokea
Hali ilivyokuwa baada ya mlipuko ulioua na kujeruhi vibaya
Hali za majeruhi na marehemu wakiwa chini kabla ya kukimbizwa hospitalini
FUNUN HABARI REPORTER ARUSHA- MOSES BENDERA.
PICHA KWA HISANI-libeneke noise of silence
Kwa habari zaidi ungana nasi Tena Hapa hapa Tunakujuza.

This post was written by: Author Name
Author description goes here. Author description goes here. Follow him on Twitter
Get Updates
Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.
Related Articles
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



1 Responses to “Picha : Baaadhi ya Picha za Matukio Bomu lilolipuka Baada ya Mkutano Wa Chadema Kaloleni Arusha leo.”
June 15, 2013 at 1:06 PM
amani amani tz
Post a Comment
Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.