Monday, June 10, 2013

TCRA YAAGIZA STAR TV IRUDISHWE MARA MOJA KATIKA VING'AMUZI VYA STAR TIMES



Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Prof. John Nkoma akitoa maamuzi kuhusu kujitoa kwa Star TV kwenye Star Times. 

TCRA imeagiza Chaneli ya Star Tv irudishwe mara moja kwenye Star Times ndani ya masaaa machache yajayo. 

Aidha Star Times na Star TV wameelezwa kuwa wote wamevunja sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta ya 2010 na Kanuni zake na kutakuwa na kujitetea tarehe 17 Juni 2013. 

Agizo la kurudishwa kwa Chaneli ya Star TV linatakiwa kutekelezwa ili kuhakikisha kuwa wananchi hawanyimwi haki ya kupata habari. 

Vile vile wote wametakiwa kufuata Sheria inapotokea kutokuafikiana badala ya kutoa maamuzi bila kumshirikisha Mdhibiti (TCRA)

Tags:

0 Responses to “TCRA YAAGIZA STAR TV IRUDISHWE MARA MOJA KATIKA VING'AMUZI VYA STAR TIMES ”

Post a Comment

Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.

HHHHHHHHHHHH

Subscribe

Kwa habari na Taarifa weka Email yako Hapa tutakutumia

© 2014 FUNUNU HABARI.. All rights reserved.
Designed by FUNUNU HABARI