Friday, July 19, 2013

Breaking News!!!! Manchester United inatarajia hii habari njema ndani ya saa 48.



Taarifa iliyonukuliwa toka kwenye gazeti la The Daily Mail la England inasema club ya Manchester United inatarajia kupata habari njema ya usajili wa kiungo wa Barcelona Francesc Fabregas ndani ya saa 48 zijazo.

Mkurugenzi wa Manchester United ambaye pia ni makamu wa rais wa klabu hiyo Ed Woodward alikatisha safari yake huko Australia ambako aliambatana na United iliyoweka kambi kwa ajili ya mchezo mmoja wa kirafiki na inasemekana kuwa safari yake hiyo ya ghafla kurudi England ilikuwa kukamilisha usajili wa mchezaji anayeaminika kuwa Cesc Fabregas.

Awali kocha wa Barcelona Tito Villanova alisema kuwa mchezaji huyo ana nafasi kwenye kikosi cha Barca na hatazamii kama klabu hiyo itampoteza lakini uongozi wa Barcelona una mtazamo tofauti na ule wa kocha Tito ambapo rais wa Barca Sandro Rossel yuko tayari kusikiliza ofa za mchezaji huyo kwani Barcelona wanahitaji kutengeneza fedha.


Katika hali ya kawaida Fabregas amekuwa na nafasi kwenye kikosi cha Barcerlona japo si nafasi ya kiungo ambayo anapenda kucheza ambapo kusajiliwa kwa mchezaji wa kimataifa toka Brazil Neymar, kunaweza kupunguza nafasi ya Cesc kwenye kikosi cha kwanza hasa katika kipindi hiki ambapo michuano ya kombe la dunia inakaribia.

United wanaweza kupata upinzani kwenye harakati za kumsajili Fabregas toka Arsenal ambayo ina makubaliano na Barca ya kuwa timu ya kwanza kupewa fursa ya kumsajili kiungo huyo ambae alikuwa nahodha wao wa zamani.

Mashabiki wa United bado wanaugulia machungu ya kumkosa kiungo mwingine wa Hispania Thiago Alcantarra ambaye alichagua kusajiliwa Bayern japo alidhaniwa kuwa yuko karibu kujiunga na Man United.

Story za Michezo hapa millardayo.com ni kwa nguvu ya NMB, chukua pesa yako popote kwenye ATM zaidi ya 500 Tanzania, kwa siku unaweza kuchukua mpaka shilingi milioni moja.
miladayo.com

Tags:

0 Responses to “ Breaking News!!!! Manchester United inatarajia hii habari njema ndani ya saa 48. ”

Post a Comment

Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.

HHHHHHHHHHHH

Subscribe

Kwa habari na Taarifa weka Email yako Hapa tutakutumia

© 2014 FUNUNU HABARI.. All rights reserved.
Designed by FUNUNU HABARI