Friday, July 19, 2013
MMILIKI WA HOME SHOPPING CENTRE AMWAGIWA TINDIKALI
Friday, July 19, 2013 by Unknown
HABARI ZIMETUFIKIA PUNDE TU ZINASEMA MFANYABIASHARA MMOJA MAARUFU NCHINI AMEMWAGIWA KITU KINACHODHANIWA NI TINDIKALI NA WATU WASIOJULIKANA MAENEO YA MSASANI JIRANI NA KITUO CHA POLISI CHA OYSTERBAY JIJINI DAR ES SALAAM.
JINA LA MFANYABIASHARA HUYO BADO HALIJAJULIKANA, NA HATA POLISI BADO HAWAJAKANUSHA WALA KUTHIBITISHA TUKIO HILO LINALOSEMEKANA LILILOTOKEA BAADA YA MUDA WA KUFUTURU KUMALIZIKA.
AIDHA, WANAHABARI WETU WAMESHUHUDIA MAGARI KADHAA YA POLISI YAKIWA KWENYE MAEGESHO YA DUKA MOJA KUBWA LILILOPO MAENEO KARIBU NA OYSTERBAY POLICE, AMBAKO HAKUNA ALIYETAKA KUSEMA CHOCHOTE, JAPO HABARI ZINASEMA HAPO NDIPO TUKIO LILIPOTOKEA.
JUHUDI ZA KUMSAKA KAMANDA WA POLISI MKOA WA KINONDONI AMA KAMANDA WA KANDA MAALUMU YA DAR ES SALAAM AFANDE SULEIMAN KOVA ZINAENDELEA. NASI TUTAWAJULISHA KILA TUTAPOPATA HABARI ZAIDI.
Taarifa za awali zinadai kwamba Mfanyabiashara Said Mohamed Saad ambaye ni Mmiliki wa Home Shopping Centre (Dar), amwagiwa tindikali saa mbili ya usiku huu maeneo ya Msasani City Mall ....
Taarifa hizo zinadai kwamba mtuhumiwa aliyefanya kitendo hicho alitoka mbio, mlinzi akamkimbiza lakini bahati mbaya akateleza na kuanguka na jamaa akawahi pikipiki na kutoweka eneo la tukio,
Source: Michuzi Blog
Tags:
kitaifa

This post was written by: Author Name
Author description goes here. Author description goes here. Follow him on Twitter
Get Updates
Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.
Related Articles
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

0 Responses to “MMILIKI WA HOME SHOPPING CENTRE AMWAGIWA TINDIKALI ”
Post a Comment
Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.