Monday, July 15, 2013

JOHN TENDWA AZUNGUMZIA KWA VYAMA VYA SIASA



OFISI ya Msajili wa Vyama Vya Siasa nchini imevitaka vyama vya siasa kutii agizo la kutoanzisha kambi za mafunzo ya kulinda amani maarufu kwa jina la mgambo , huku ikisisitiza kwamba itachukua hatua za kisheria kwa chama chochote kitakachoiuka , ikiwemo kukifuta.

Aidha ofisi hiyo imesema kuwa Katiba ya nchi imempa jukumu kila mwananchi kulinda amani na usalama wa nchi, pia kujilinda yeye mwenyewe na mali zake kwa kutoa taarifa katika vyombo vya dola pale anaposikia au kuona mtu anataka kufanya au anafanya uhalifu au amemdhuru mtu.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dares Salaam na ofisi hiyo katika taarifa yake iliyoitoa kwa vyombo vya habari iliyotiwa saini na Rajab Juma kwa niaba ya Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini, John Tendwa kufutia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutangaza hivi karibuni kinakusudia kuanzisha kambi za mafunzo ya kujilinda kwa vijana wake nchi nzima.

Alisema suala hilo lilitangazwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe na kuandikwa katika vyombo vya habari kabla ya chama hicho, kuwasiliana na taasisi husika ikiwemo ofisi hiyo ili kupata ushauri kuwa 




jambo wanalotaka kufanya ni sahihi.

“Hivyo Katiba ya nchi na katiba za za vyama vya siasa, hazina maana kila mwananchi au kikundi fulani wafanye mafunzo ya kijeshi au ukakamavu ili kufanikisha jukumu hili.

“Jukumu la vikundi kama hivi ni kutoa taarifa kwa vyombo vya dola na si kupambana na wahalifu au watu wanaotaka kuwadhuru wenye jukumu la kupambana na wahalifu ni vyombo vya ulinzi na usalama ambavyo vipo kisheria, mojawapo ikiwa ni Jeshi la Polisi,” alisema Juma.

Juma alikitaka chama hicho na vyama vingine vinavyofikiria au kufanya jambo hilo kuacha mara moja kwani kufanya hivyo ni kukiuka Sheria za Nchi ikiwemo Sheria ya Vyama Vya Siasa ya mwaka 1992 kifungu cha 9(2)(C) cha sheria hiyo kinakataza chama cha siasa kuruhusu kutumika, kushabikia au kutumia nguvu ili kufanikisha malengo yake ya kisiasa.

Alisema chama cha siasa kutoa mafunzo ya kutumia nguvu kwa wanachama wake, ili kutekeleza jambo lolote lile ikiwamo kujilinda ni mojawapo ya masuala yanayokatazwa na Sheria ya Vyama vya Siasa.

Aliongeza kuwa kifungu cha (20) cha Sheria ya Vyama Vya Siasa kinasema uamuzi wa Msajili ni wa mwisho na hauwezi kukatiwa rufaa mahakamani.

Akizungumzia kuhusu madai kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wana kambi za mafunzo ya kupambana na vijana wake kama kisingizio cha kuvunja sheria hiyo alisema hayana msingi.

“Kama CCM wanakiuka sheria ni jukumu la CHADEMA, kila Chama na kila Mtanzania, kutoa taarifa na ikiwezekana na ushahidi katika taasisi husika, ikiwemo Ofisi ya Msajili wa Vyama Vya Siasa ili suala hili lishughulikiwe kisheria,” alisisitiza.

Msajili huyo aliviasa vyama vya siasa kutumia muda wao kufanya shughuli za siasa ili kuchangia maendeleo ya nchi, badala ya kutumia uwezo wao na muda wa kubuni mambo yanayoleta mtafaruku na kuhatarisha mani na utulivu wa nchi yetu.

“Amani ikitoweka vyama vya siasa vitakuwa katika makaratasi tu. Kutakuwa hakuna mikutano wa kamati kuu, hakuna ‘press conference’ yaani mikutano na waandishi wa habari, hakuna operesheni ya kuzunguka nchi nzima n.k. Demokrasia hutekelezwa na kukua mahali penye amani na utulivu,” alisema

Tags:

0 Responses to “JOHN TENDWA AZUNGUMZIA KWA VYAMA VYA SIASA ”

Post a Comment

Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.

HHHHHHHHHHHH

Subscribe

Kwa habari na Taarifa weka Email yako Hapa tutakutumia

© 2014 FUNUNU HABARI.. All rights reserved.
Designed by FUNUNU HABARI