Wednesday, February 26, 2014

HII KALI DAKTARI FEKI MWINGINE AKAMATWA MUHIMBILI



Jana February 25 Uongozi wa hospitali ya taifa muhimbili kwa kushirikiana na maafisa wake wa usalama wamemnasa daktari feki aliyekuwa akiwatapeli fedha wagonjwa na watu mbalimbali wanaofika kwa ajili ya kupatiwa huduma za matibabu katika hospitali hiyo.
Taarifa kutoka Muhimbili inasema ni Tukio la tatu kutokea katika hospitali hiyo ingawa matukio ya namna hiyo yameshawahi kuripotiwa katika baadhi ya hospitali kubwa za serikali kwa baadhi ya watu wanaotumia mwavuli wa fani ya udaktari kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.
Msemaji wa Hospital ya taifa Muhimbili Aminieli Aligaesha amemtaja Daktari huyo feki kwa jina la Kitano Mustapha na kubainisha kuwa katika upekuzi uliofanywa na maofisa usalama wa hospitali hiyo wamemkuta mtuhumiwa akiwa na kadi tatu za kliniki,namba za simu za madaktari na wauguzi katika hospitali hiyo huku wakitambua kufanya hivyo ni kosa kwa mujibu wa sheria zilizopo na kanuni za utabibu.
Daktari huyo feki Kitano Mustapha amekana kutohusika na utaperi huo kwa wagonjwa mbali mbali wanaofika kupata huduma za kimatibabu na kusema hawezi kuongea lolote mpaka Mwanasheria wake awepo.

Tags:

0 Responses to “HII KALI DAKTARI FEKI MWINGINE AKAMATWA MUHIMBILI”

Post a Comment

Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.

HHHHHHHHHHHH

Subscribe

Kwa habari na Taarifa weka Email yako Hapa tutakutumia

© 2014 FUNUNU HABARI.. All rights reserved.
Designed by FUNUNU HABARI