Sunday, February 23, 2014
MREMBO AIBA SIMU NA KUIFICHA SEHEMU ZA SIRI: APEWA KICHAPO CHA HATARI
Sunday, February 23, 2014 by Unknown
MREMBO mmoja mkazi wa Mabibo Makutano jijini Dar es Salaam (jina lake halikupatikana) mwishoni mwa wiki iliyopita alinusurika kifo baada ya kuvamiwa na kudundwa baada ya kudaiwa kukwapua simu ya mwanaume na kuificha sehemu zake za siri.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, awali mrembo huyo alikuwa akila bata na mwanaume aitwaye Hashim kwenye Baa ya Jassun Inn iliyopo maeneo ya Mabibo huku mwanaume huyo akiwa ametandaza simu zake za kisasa juu ya meza.
Imedaiwa kuwa wakati wakiendelea kuponda raha, Hashim alikwenda msalani kwa lengo la kujisaidia na kuacha simu zake mezani, aliporudi hakumkuta mrembo aliyekuwa akiponda naye raha na simu yake moja haikuwepo.
Jasho lilimtoka Hashim na kuwauliza watu waliokaa jirani alikoelekea mrembo huyo,” alisema shuhuda mmojawapo wa tukio hilo na kubainisha kwamba msamaria mwema mmoja alimweleza Hashim mwelekeo wa mrembo huyo.
Bila kuchelewa Hashim aliwakusanya wapambe wake na kuanza kumtafuta mrembo huyo na wakamnasa mita kama 150 kutoka Baa ya Jassun na kumuuliza kuhusu simu iliyokuwa mezani lakini alileta ubishi.
- GPL
Tags:
udaku

This post was written by: Author Name
Author description goes here. Author description goes here. Follow him on Twitter
Get Updates
Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.
Related Articles
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MREMBO AIBA SIMU NA KUIFICHA SEHEMU ZA SIRI: APEWA KICHAPO CHA HATARI”
Post a Comment
Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.