Friday, March 14, 2014
"MPENZI TUJENGE NYUMBA MBILI TUKIACHANA KILA MTU ACHUKUE YAKE"
Friday, March 14, 2014 by Unknown
Unawezaje kumwambia mumeo tena wa ndoa maneno kama hayo? mweeee!
Maneno haya kaambiwa mwanaume na mkewe wa ndoa wiki moja iliyopita.
Kwa sasa jamaa hamuamini kabisa mkewe akihofia huenda huyu mwanamke atakuja kumuua kwa sababu ya mali.
Wakiwa sebuleni baada ya kula mwanamke-ghafla tu-akamwambia mumewe eti wajenge nyumba nyingine ya pili ili ikitokea huko mbeleni wakiachana basi kila mmoja awe na nyumba yake kwani hii nyumba wanayoishi sasa mwanaume alijenga kabla ya kumuoa yeye.
Mwanamke anahofia hatapata kitu ikitokea atakufa au wakiachana huko mbeleni.
Mshikaji kaja niambia afanyeje, maana anahofia huenda huyu mwanamke anaweza kuja kumtoa roho kama watakuja kuwa na mali.
Sababu ya hofu hii, mshikaji anafikiria hata kukiuza kiwanja chake kilichopo bunju alichokuwa anapanga kuanza ujenzi mwezi wa nane.
Hivi jamani mkeo akikwambia maneno kama haya, na ndo hivyo ushamuoa kwa ndoa ya kanisani utafanyaje? Tags: mapenzi

This post was written by: Author Name
Author description goes here. Author description goes here. Follow him on Twitter
Get Updates
Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.
Related Articles
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

0 Responses to “"MPENZI TUJENGE NYUMBA MBILI TUKIACHANA KILA MTU ACHUKUE YAKE" ”
Post a Comment
Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.