Wednesday, March 27, 2013

Anayedaiwa Kumgonga askari wa Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani(Trafiki), Elikiza Nnko Nakusababisha Kifo Huyu Hapa Apandishwa Kizimbani


Mtuhumiwa anayedaiwa  kumgonga na kumuua askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Koplo Elikiza Nnko, Jackson Simbo akipandishwa kizimbani  katika  Mahakama ya Hakimu Mkazi  Kinondoni jijini Dar es Salaam jana.Picha na Michael Jamson  
--
Dereva Jackson Simbo (43), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, kujibu shtaka la kusababisha kifo cha askari wa Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani, Elikiza  Nnko.Mshtakiwa huyo, alifikishwa mahakamani jana.

Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Ladislous  Komanya, alidai kuwa mshtakiwa alitenda makosa hayo Machi 18 mwaka huu, katika  eneo la Bamaga, Barabara ya Bagamoyo.
Wakili Komanya alidai kuwa  pamoja na shtaka  hilo, mshtakiwa  pia anakabiliwa na shtaka la kuingilia msafara wa kiongozi, kinyume na sheria. Wakili alidai kuwa akiwa katika sehemu hiyo ya  Bamaga, mshtakiwa  aliingilia msafara wa kiongozi na kushindwa kuheshimu maelekezo yaliyokuwa yakitolewa kwa ishara na askari huyo.
Komanya  aliendelea kudai,  Simbo pia anakabiliwa na  shtaka la  shindwa kutoa taarifa katika kituo chochote cha polisi hadi alipo tafutwa na vyombo vya dola.Kwa Habari zaidi Bofya na Endelea....>>>>

Tags:

0 Responses to “Anayedaiwa Kumgonga askari wa Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani(Trafiki), Elikiza Nnko Nakusababisha Kifo Huyu Hapa Apandishwa Kizimbani ”

Post a Comment

Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.

HHHHHHHHHHHH

Subscribe

Kwa habari na Taarifa weka Email yako Hapa tutakutumia

© 2014 FUNUNU HABARI.. All rights reserved.
Designed by FUNUNU HABARI