Thursday, April 11, 2013

TFF Kuwakata simba Hela Kila Mechi Kumlipa Victor Costa Mil 28


SHIRIKISHO la soka Tanzania (TFF), limesema litakuwa likikata fedha za Simba kila mechi kufikia Sh28 milioni kwa ajili ya kumlipa Victor Costa.

Kauli hiyo ya TFF imekuja, baada ya kubaini kuwa Simba imekiuka makubaliano na kuvunja mkataba na beki wake mkongwe Victor Costa bila kumlipa haki zake za msingi.

Costa alisajiliwa na Simba kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Msumbiji, lakini amekuwa akisumbiliwa na maumivu ya goti kwa kipindi kirefu sababu ambazo zilielezwa kuwa ndicho chanzo cha

Wekundu hao kukatisha mkataba wake. Simba ilitaka kumtoa kwa mkopo wakati wa usajili dirisha dogo lakini mchezaji huyo alikataa na kuomba kukatisha mkataba wake uliokuwa umebakia miezi 18 kabla ya kumalizika.

Costa alisema hivi karibuni jijini Dar es Salaam kuwa anidai Simba Sh28 milion ikiwa ni malimbikizo ya mishahara yake na bonus.

Chanzo hicho kilieleza kuwa Simba walikubali na kuahidi kumlipa mshahara kila mwezi kwani hawakuwa na uwezo wa kumlipa fedha zote kwa mara moja.

Lakini, tangu walipokubaliane hadi sasa Simba hawajamlipa hata shilingi moja na kufanya mchezaji huyo kwenda kuwashtaki TFF na kuamua mchezaji huyo alipwe kupitia mapato ya milangoni kwa kila mechi watakazocheza.

Victor Costa alivyotafutwa kuzungumzia suala hilo alisema;
"Siwezi kuzungumza lolote kwa sasa. Nafikiri kazi nimewaachia TFF waweze kunisaidi kulipwa haki zangu."

Kwa upande wa Simba, Ofisa habari wao, Ezekiel Kamwaga amekiri ni kweli klabu hiyo inadaiwa na beki huyo;

"Tumekwisha wasiliana na Costa kumwahidi kuwa asiwe na shaka tutamlipa fedha zake zote." alisema Kamwaga.

Tags: ,

0 Responses to “TFF Kuwakata simba Hela Kila Mechi Kumlipa Victor Costa Mil 28”

Post a Comment

Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.

HHHHHHHHHHHH

Subscribe

Kwa habari na Taarifa weka Email yako Hapa tutakutumia

© 2014 FUNUNU HABARI.. All rights reserved.
Designed by FUNUNU HABARI