Tuesday, May 7, 2013

TAARIFA KWA UMMA

TAARIFA KWA UMMA





Kampala International University, Dar es Salaam Constituent College (KIU-DCC)

KUSIMAMISHWA KWA MAFUNZO YA SHAHADA ZA UZAMILI NA UZAMIVU 

Kampala International University, Kampasi ya Dar-es-Salaam (KIU-DCC) kilichopo Gongo la 

Mboto, Dar-Es-Salaam ni Chuo kilichopewa idhibati na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania

(TCU). 

Kufuatia kuendesha mafunzo ya shahada ya Uzamili (Masters) na Shahada za Uzamivu 

(PhD) kinyume cha utaratibu na kutokua na wahadhiri wa kutosha wenye sifa stahili, Tume 

katika mkutano wake wa hivi karibuni ulikiamuru Kampala International University, 

Kampasi ya Dar-es-Salaam ifuatayo;

1. KIU isimamishe mara moja mafunzo yote ya shahada za juu (Postgraduate) ikuwa ni 

pamoja na Shahada za Uzamili (Masters) na Shahada za Uzamivu (PhD) katika 

kampasi ya Dar-es-Salaam

2. KIU ishirikiane na wanafunzi wote iliyowadahili katika programu zilizotajwa hapo 

juu waweze kuhamia kwenye vyuo vingine vyenye idhibati ya kutoa mafunzo hayo.

Tume haitatambua shahada yeyote ya Uzamiili au Uzamivu itakayotolewa na chuo hicho 

kwa watakaosoma katika kampasi ya Dar-es-Salaam. 

Angalizo:

Chuo cha KIU Kampasi ya Dar-es-Salaam kina ithibati na kitaendelea kutoa mafunzo ya 

shahada ya kwanza (Bachelors), Diploma au vyeti zilizopitishwa na TCU kwa mujibu wa

Ithibati ya Chuo Husika.

Imetolewa na:

Katibu Mtendaji

TUME YA VYUO VIKUU TANZANIA (TCU)

Tags:

0 Responses to “TAARIFA KWA UMMA ”

Post a Comment

Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.

HHHHHHHHHHHH

Subscribe

Kwa habari na Taarifa weka Email yako Hapa tutakutumia

© 2014 FUNUNU HABARI.. All rights reserved.
Designed by FUNUNU HABARI