Friday, June 28, 2013
JK: Tanzania itanufaika uhusiano na Sri Lanka
Friday, June 28, 2013 by Unknown
Rais Jakaya Kikwete
|
RAIS Jakaya Kikwete amewahakikishia Watanzania kuwa watafaidika na uhusiano wa Tanzania na Sri Lanka hasa katika masuala ya uchumi, biashara na utalii .
Aliyasema hayo baada ya Tanzania na Sri Lanka kutiliana saini mikataba mitatu ya ushirikiano katika masuala ya uchumi, ufundi, utamaduni, michezo na utalii.
Hafla ya utiaji saini ilifanyika usiku wa juzi katika Ikulu ya Dar es Salaam ambapo, Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Bernard Membe na wa Sri Lanka, Profesa G.L. Peiris, huku wakishuhudiwa na marais, Jakaya Kikwete na Mahinda Rajapaksa wa Sri Lanka.
Akizungumza katika hafla ya chakula cha usiku Ikulu Dar es Salaam juzi, Rais Kikwete alisema Sri Lanka imesonga mbele na kurudisha uchumi wake ulioyumba kutokana na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe kwa miaka 30 na kwamba, imekuwa na mbinu nzuri za kujiletea maendeleo hasa kiuchumi kiasi cha kuivutia Tanzania.
“Nawapongeza watu wa Sri Lanka kwa sababu wameweza kurejesha hali nzuri ya amani katika nchi yao. Naamini amani hiyo itaendelea kudumu. Uchumi wao ni wa kutia moyo na wenye kutamanisha kutokana na ukweli kwamba umekua kwa haraka ndani ya muda mfupi”, Rais alisema na kuongeza kuwa hata sekta ya utalii ya nchi hiyo ipo juu sana sasa.
Kwa mujibu wa Rais, kwa mwaka jana pekee iliweza kujiingizia watalii wasiopungua milioni moja katika vipindi vya mapumziko na kwamba, watu hao walikuwa wakitembelea zaidi fukwe za nchi hiyo na kuifanya irudie katika enzi zake za kujiwa na wageni wengi waliokuwa wakichangia kukuza kipato cha taifa hilo kupitia sekta ya utalii.
Alibainisha pia kuwa Sri Lanka sio ngeni kwa Tanznaia kutokana na ukweli kwamba raia wake wamekuwa wakija Dar es Salaam na hata kuweza kupanda mti uliodumu kwa miaka mingi pamoja na kuitambulisha Budha kwa kujenga Hekalu la Kibudha miaka 93 iliyopita.
NA HABARI LEO.
Tags:
kitaifa

This post was written by: Author Name
Author description goes here. Author description goes here. Follow him on Twitter
Get Updates
Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.
Related Articles
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “JK: Tanzania itanufaika uhusiano na Sri Lanka ”
Post a Comment
Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.