Tuesday, March 19, 2013
SAMATTA, ULIMWENGU WAWASILI KUIKABILI TIMU YA MOROCCO
Tuesday, March 19, 2013 by Unknown



…………………………………………………………………
Na Mwandishi wetu
Wachezaji wa Timu ya Taifa (Taifa Stars), Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wanaoichezea TP Mazembe ya DRC wamewasili Jumatatu jioni na kujiunga na wachezaji wenzao tayari kwa maandalizi ya kuikabili Morocco katika mechi ya kuwania kucheza Fainali za Kombe la Dunia mwakani.
Wachezaji hao, ambao ni tegemeo kubwa katika TP Mazembe wamewahakikishia watanzania ushindi Jumapili hii na kuwataka wajitokeze kwa wingi kuishangilia timu yao ya Taifa.
Samatta na Ulimwengu wamewasili nchini wakitokea Nchini Boswana walikokuwa na Timu yao ya TP Mazembe.
Akizungumza mara baada ya kuwasili, Samata alisema ushindi dhidi ya Morocco ni lazima, hivyo Watanzania wasiwe na hofu na timu yao na wao wako tayari kuliongoza jahazi hilo la ushindi.
“Tumekuja kuungana na wachezaji wenzetu wa Timu ya Taifa, tumekuja kuhakikisha timu yetu inashinda na tuna kila sababu ya kushinda maana tunacheza nyumbani,” alisema Samatta ambaye aliifungia Tanzania bao la ushindi dhidi ya Cameroon mapema mwaka huu.
Alisema kuwa wao wako fiti na hawana tatizo lolote na wanajiunga na kambi usiku huo huo waliowasili na kuanza mazoezi kama ratiba ilivyo pangwa na hivyo watanzania wajiandae kushangilia ushindi.
Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inayodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro lager, imeingia kambini tangu Jumamosi ilitarajiwa kuanza mazoezi jana Jumanne baada ya wachezaji wote 23 walioitwa kuripoti kambini.
Kocha wa timu ya Taifa, Kim Poulsen amekwishasema kuwa hana wasiwasi na Morocco kwani ameshawasoma na kuona mchezo wao wakati wa Kombe la Afrika na juzi wakati Morocco ilicheza na Mali kwa hivyo anajua namna ya kuwaandaa wachezaji wake kukabiliana nao.
Taifa Stars iko katika kundi moja na Ivory Coast, Morocco na Gambia huku Ivory Coast ikiongoza kwa pointi nne, Tanzania ya pili na pointi tatu, Morocco pointi mbili na Gambia pointi moja.
Ushindi katika mechi hii itawapa wachezaji na Watanzania ari ya kusonga mbele zaidi
Tags:
kitaifa ,
michezo

This post was written by: Author Name
Author description goes here. Author description goes here. Follow him on Twitter
Get Updates
Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.
Related Articles
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “SAMATTA, ULIMWENGU WAWASILI KUIKABILI TIMU YA MOROCCO ”
Post a Comment
Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.