Thursday, May 2, 2013
Kagasheki amkingia kifua Kinana
Thursday, May 2, 2013 by Unknown

Balozi Kagasheki alikuwa anajihusisha na masuala ya kusafirisha meno ya tembo baada ya meli iliyofanyiwa kazi na Kampuni ya Sharaf kukamatwa nchini China ikisafirisha meno hayo.
Kagasheki alisema ni makosa kwa Kinana kutuhumiwa wakati kilichokuwa kimebebwa kwenye meli hiyo hakikuwa mali yake.
“Hivi ina maana wamiliki wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) au wale wa Precission Air ndiyo wanapaswa kutuhumiwa kwa kile kinachobebwa na abiria wao kweli?
Ndugu yangu Mchungaji Msigwa anafahamu ninamheshimu sana. Ingawa amenirushia makombora mengi sana. Lakini katika hili nadhani hata kama ni siasa nadhani ni kitu ambacho hakikubaliki kwa wastaarabu,” alisema.
Hata hivyo, Balozi Kagasheki aliahidi kuwa Serikali imepanga kufanya operesheni dhidi ya majangili wa meno ya tembo.
Alisema hawatatangaza siku ya operesheni hiyo kutokana na kuwahusisha watu wengi.
Loliondo
Kuhusu mgogoro wa siku nyingi wa Loliondo, Balozi Kagasheki aliahidi kuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda atatolea ufafanuzi suala la eneo tengefu la Loliondo wakati wowote katika kipindi hiki cha Bunge la Bajeti.
Alisema Serikali imeshughulikia kwa nia njema suala hilo lakini kutokana na malalamiko ya wananchi kufikishwa kwa Waziri Mkuu, wanasubiri uamuzi wake.
Loliondo kuna mvutano mkubwa kutokana na wananchi kupinga mpango wa Serikali kutwaa hekta 1,500 za mraba kutoka katika ardhi ya vijiji kama eneo tengefu.
Tags:
kitaifa

This post was written by: Author Name
Author description goes here. Author description goes here. Follow him on Twitter
Get Updates
Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.
Related Articles
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “Kagasheki amkingia kifua Kinana ”
Post a Comment
Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.