Friday, May 10, 2013

Makamba atapeliwa, kutapeli wasanii



Naibu Waziri, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,January Makamba akifafanua jambo Dar es Salaam,Tanzania

JINA la Naibu Waziri, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia January Makamba linatumiwa na matapeli kutapeli wasanii wa muziki na sanaa ya maigizo nchini.

Genge la matapeli hao wamefanikiwa kumtapeli Naibu Waziri huyo kwa kutumia jina lake ili litumike kutapeli wasanii pamoja watu malimbali nchini.

Mbunge huyo wa Bumbuli amehusishwa na genge hilo linalojitangaza kwa wasanii, kuwa ni asasi ya kuinua vipaji vya sanaa nchini Tanzania, huku akitajwa kuwa ndiyo mmiliki wake.

Asasi hiyo feki iliyojaa utapeli wa hali ya ijuu imekuwa ikiwatapeli wasanii mbalimbali inchi humo ikiwemo vikundi vya sanaa ya maigizo,huku wakijitambulisha kwa jina la Zinduka Foundation na tovuti yao nihttp://www.zindukafoundation.wapka.mobi/index.html ambayo imeondolewa hewani dakika chache baada ya Habarimpya.comkutangaza taarifa hizi. Taarifa za utapeli wa asasi hiyo imenaswa na Habarimpya.com na baadaye Naibu Waziri huyo akaandika kwenye ukurasa wake wa Face Book kwa lengo la kuwatahadharisha wananchi. "Ndugu zangu, kuna asasi inajiita Zinduka Foundation ambayo imekuwa ikiwatapeli watu mbalimbali na ikijitangaza kama asasi ya kuinua vipaji vya sanaa ya muziki na maigizo hapa nchini. Asasi hiyo feki inajitangaza kwamba mimi ndiye mmiliki wake" alisema Makamba na kuongeza:.

"(Nimeambatanisha tovuti yao). Ndugu zangu, hawa ni matapeli na nawatahadharisha kuwa makini kupitia ujumbe huu. Wanatumia namba 0652206173 ambayo wameisajili kwa jina Omari Makamba. Watu hawa ni matapeli, sihusiki na jambo hili kwa namna yoyote ile na tayari nimetoa taarifa kwa vyombo husika".

Tags: ,

0 Responses to “Makamba atapeliwa, kutapeli wasanii”

Post a Comment

Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.

HHHHHHHHHHHH

Subscribe

Kwa habari na Taarifa weka Email yako Hapa tutakutumia

© 2014 FUNUNU HABARI.. All rights reserved.
Designed by FUNUNU HABARI