Sunday, May 5, 2013

Mbunge Nassari Akitoa Damu Kuwapa Majeruhi wa Mlipuko wa Bomu Arusha

Nassari Akitoa damu kwa Majeruhi Mlipuko wa Bomu
Mbunge wa Arumeru Mashariki, Jushua Nassari mbali ya kuwahamasisha watu kutoa damu, pia hivi punde amemaliza kutoa damu kwa ajili ya kuwachangia majeruhi waliolipukiwa na bomu kanisani LEO. Pichani Nassari akionekana akitoa damu kwa ajili ya kuwawekea majeruhi.

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema na Mbunge wa Arumeru Mashariki, Jushua Nassari LEO tangu majira ya saa 5:30 asubuhi wamekuwa wakifanya kazi ya kuwahamasisha watu kutoa damu kwa ajili ya kuwawekea majeruhi mbalimbali waliojeruhiwa na bomu katika kanisa la Parokia Mpya ya Olasiti mjini humo.

Kutokana watu wengi kupoteza damu na kumwagika kwa wingi. Mbali na hilo baadhi ya wahudumu wa hospitali hiyo wameueleza mtandao wa Habarimasai.com kwamba hivi sasa wana wakati mgumu katika kufanya usafi na mwandishi wetu Joseph Pantaleo ameshuhudia manesi hao wakisafisha damu sakafuni kila wakati huku wakimwaga maji na dawa ili kuondoa mabaki ya damu hiyo.

Lema na Nassari wameonekana wakiwahamisisha watu kutoa damu na wengi wameitikia wito huo. Endelea kusoma habarimasai.com kwa taarifa

Tags:

0 Responses to “Mbunge Nassari Akitoa Damu Kuwapa Majeruhi wa Mlipuko wa Bomu Arusha ”

Post a Comment

Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.

HHHHHHHHHHHH

Subscribe

Kwa habari na Taarifa weka Email yako Hapa tutakutumia

© 2014 FUNUNU HABARI.. All rights reserved.
Designed by FUNUNU HABARI