Sunday, May 5, 2013

Updates: Tukio la Mlipuko wa Bomu katika Ufunguzi wa kanisa la St. Joseph Parokia ya Olasiti Arusha






Kwa sasa hali ya kawaida inaanza kurudi. Vyombo vya usalama vinaendelea kuchunguza ili kujua mlipuko huo ni nini hasa.
Balozi wa papa nchini na viongozi wa juu wa jimbo wameondoka eneo la tukio salama na balozi hajadhurika kabisa ingawa mlipuko huo ulilipuka karibu nao.
Mkuu wa mkoa alikuja na sasa ameondoka.
Wananchi wameanza kupungua eneo la tukio na wengi wanaelekea Mount Meru ili kuwatambua majeruhi. Hivyo idadi ya watu wanaondoka eneo la tukio na kwenda hospitali.
Polisi wamekamata pikipiki ambayo inasadikiwa imetumika katika tukio hilo.
Shughuli ya uzinduzi wa kanisa hilo imeahirishwa hadi tarehe ambayo haijatajwa
Mungu awajalie majeruhi wapate nafuu haraka.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Tags:

0 Responses to “Updates: Tukio la Mlipuko wa Bomu katika Ufunguzi wa kanisa la St. Joseph Parokia ya Olasiti Arusha ”

Post a Comment

Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.

HHHHHHHHHHHH

Subscribe

Kwa habari na Taarifa weka Email yako Hapa tutakutumia

© 2014 FUNUNU HABARI.. All rights reserved.
Designed by FUNUNU HABARI