Friday, June 21, 2013
Inasemekana Dida Wa Clouds FM Anusurika Kifo
Friday, June 21, 2013 by Unknown
Khadija Shaibu ‘Dida’.
Na Imelda Mtema
MTANGAZAJI wa Radio Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida’ amefungua kinywa chake na kusema ugonjwa wa malaria uliompata hivi
karibuni ulimfanya alichungulie kaburi kwani alihisi mauti yanamkuta.
Akizungumza na paparazi wetu mapema wiki hii katika Hospitali ya Muhimbili, jijini Dar, Dida alisema kitendo cha kukutwa na malaria 250 katika mwili wake kilikuwa hatari sana kwani ingeweza kumuondoa uhai kabisa.
“Nilichungulia kaburi mwenzenu maana hali niliyokuwa naisikia siku ile ya kwanza ilikuwa ni nusu duniani, nusu akhera. Nilikuwa wa leo au wa kesho ila namshukuru Mungu kwa sasa naendelea vizuri,” alisema Dida.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, Dida alipandwa na malaria kali, akakimbizwa katika Hospitali ya Amana, Ilala jijini Dar kisha kuhamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu zaidi.

This post was written by: Author Name
Author description goes here. Author description goes here. Follow him on Twitter
Get Updates
Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.
Related Articles
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “Inasemekana Dida Wa Clouds FM Anusurika Kifo ”
Post a Comment
Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.