Wednesday, June 19, 2013
Mahakama Ya Hakimu Mkazi Kisutu Yamwachia Huru, Iddy Simba Jijini Dar Es Saalaam.
Wednesday, June 19, 2013 by Unknown

Idd Simba
Na Happiness Katabazi
HATIMAYE Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, hivi punde imemwachiria huru Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA), Idd Simba, Mkurugenzi wa Bodi hiyo ambaye alikuwa Diwani wa Kata Sinza (CCM), Salum Mwaking’inda, Meneja Mkuu wa shirika hilo Victor Milanzi na Mkurugenzi wa Kampuni ya Simon Group , Simon Kisena waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi wa shirika hilo kwa sababu Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Dk.Eliezer Feleshi kuwasilisha hati ya kutokuwa na haja ya kuendelea kuwashitaki washitakiwa hao chini ya kifungu cha 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002.
Simba anayetetewa na wakili maarufu nchini Alex Mgongolwa walifikishwa na mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Mei 27 mwaka jana wakikabiliwa na makosa ya kula njama,matumizi mabaya ya madaraka na kughushi na hujumu uchumi.
Hivyo kuanzia sasa washitakiwa hao wapo huru.
Na Juma Mtanda
Tags:
kitaifa ,
siasa

This post was written by: Author Name
Author description goes here. Author description goes here. Follow him on Twitter
Get Updates
Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.
Related Articles
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “Mahakama Ya Hakimu Mkazi Kisutu Yamwachia Huru, Iddy Simba Jijini Dar Es Saalaam.”
Post a Comment
Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.