Sunday, July 7, 2013
AIBU: AFUMANIWA GUEST HOUSE AKIWA NA MUME WA MTU..! ALA KICHAPO CHA KUFA MTU....!!
Sunday, July 7, 2013 by Unknown

Fumanizi hilo lilibuliwa ambapo Judith Lekule na mume wa mwanamke aliyetambuliwa kwa jina moja la Pendo

Kwa mujibu wa vyanzo, Judith yu mbioni kwenda kortini kwa lengo la kumfungulia mashitaka Pendo akidai alimdhalilisha kwa kudai alimfumania akiwa na mumewe.“Kuna watu wanamshawishi Judith eti asikae kimya, aende mahakamani akamshitaki Pendo kwamba alimdhalilisha kusema alimfumania na mumewe,” kilisema chanzo hicho.
Hata hivyo, vyanzo vimeeleza kwamba, Judith anashindwa kuutumia ushauri huo kutokana na ukweli kwamba, kesi hiyo inaweza kumgeukia mwenyewe kwa sababu yeye ndiye aliyefumaniwa.

Sambamba na madai hayo, inasemekana pia kwamba mtaani anapoishi Judith kumekuwa kuchungu kwake baada ya baadhi ya watu kutumia habari ya kwenye gazeti kumkejeli na kumuonya akome kuwadandia waume za watu kwani si tabia nzuri.
“Hali hiyo ya kunyooshewa vidole na watu inamnyima raha Judith, anashindwa kutembea kwa uhuru mitaani,” alisema mnyetishaji wetu.
Nao baadhi ya marafiki wa kike wa Judhith wamehuzunishwa na kitendo cha mwenzao kufumaniwa na kupewa kipigo.

Chanzo kikaenda mbele zaidi kwa kudai kwamba, ndugu wamemtaka Judith aondoke anapoishi kufuatia kitendo alichokifanya ikielezwa ameitia aibu familia.
Kwa upande wake, Pendo ameeleza kwamba mumewe alimuomba msamaha na amemsamehe, yameisha pia akasema baada ya lile fumanizi, Judith amemfuata nyumbani kwake mara mbili kwa lengo la kuomba msamaha.
“Nimemsamehe Judith lakini bado ana wasiwasi kwani amekuwa akija kwangu na hofu kwamba nitamshitaki katika vyombo vya sheria.
“Cha ajabu sasa amegeuka na kutoa vitisho, Judith ni rafiki yangu, anajua alichokifanya ndiyo maana hata wapambe wake wanamshawishi akanishitaki lakini moyo wake unakuwa mgumu,” alisema Pendo.
Tags:
mapenzi ,
udaku

This post was written by: Author Name
Author description goes here. Author description goes here. Follow him on Twitter
Get Updates
Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.
Related Articles
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “AIBU: AFUMANIWA GUEST HOUSE AKIWA NA MUME WA MTU..! ALA KICHAPO CHA KUFA MTU....!!”
Post a Comment
Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.