Sunday, July 7, 2013
NISAIDIENI JAMANI MUME WANGU ANANITESA NAONA AIBU HATA KUTOKA NJE YA NYUMBA YANGU
Sunday, July 7, 2013 by Unknown
... Dada yangu anauzunika sana!
"Nisaidieni mwenzenu jamani, nina watoto wawili, miaka 6 na miaka 4, wote wanasoma.
siku hizi mume wangu amebadilika sana, kiasi kwamba hata ada za watoto wake hatoi, hadi tugombane sana ndio anatoa ada. Mapenzi pia yamekwisha, anafanya mambo ya aibu hadharani huku watu wakiona.
Kuna siku moja alikuwa na wanawake bar, amewanunulia pombe, huku wanamshikashika, dada mmoja akiwa pale bar ananifahamu akanipigia simu niende nikamuone, nikaenda nikajionea, wanavyofanya, (walikuwa wanamtomasatomasa na kunyonyana), wanamshikashika sana kila sehemu za miili yao (na kisses nyingi). Ndipo nikapata fahamu' "ndiyo maana akirudi nyumbani anakuwa hana hamu na mimi"
Basi siku hiyo nilipata ujasiri nikamfuata pale pale, nikawambia jamani, tafuteni nyumba ya wageni, msitie aibu hapa, wale wadada walikimbia, mume wangu nae akaanza kunikimbiza ili anipige huku kashika chupa ya bia mkononi,
nikajificha mahali, nilipoona amerudi bar, nikarudi nyumbani nikachukuwa nguo nikaondoka, nikakaa kwetu mwezi mzima, badaye akaja kuomba msamaha, nilikubali nikarudi nyumbani kwa huyo mme wangu!.
Kwa sasa ujinga na upuuzi ule umeanza tena, nikimweleza atulie, anakuwa mkali na kunifokea, wakati mwingine ananitukana mbele ya watoto wangu,
"mimi naumia sana moyoni ndugu zanguni"
Mimi sina kazi, nikiondoka tu hata watoto hatawasomeshwa tena, sasa nifanyaje jamani.
Niliwahi kufungua biashara ya kutengeneza nyele (salon), akanifanyia fujo na kunifanya nifunge, hataki nifanye chochote kile,
Naomba ushauri mwenzenu, sijielewi kabisa nifanye nini, ukizingatia mtaa mzima tunakoishi wameishajua tabia yake mme wangu, naona hata aibu kutoka ndani ya nyumba."
"by Happy' she is unhappy"
*Ndugu wanaJF tumsaidieni ndugu yetu Furaha hanaraha kwa sasa.
*Yamkini kuna wadau wako kwenye mazingira kama haya ya Happy.
" Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku, kwa watu wanaoteseka kama ndugu yetu alivyosimulia tatizo linalomkabili, ili tuweza kukidhi mahitajio yake na watu wenye matatizo kama haya."
"SOMA , CHANGIA KWA KUTOA HOJA ZA KUSAIDIA NDUGU YETU NA JAMII KWA UJUMLA."
Karibu wote...
Source:Jamii forums
Tags:
mapenzi

This post was written by: Author Name
Author description goes here. Author description goes here. Follow him on Twitter
Get Updates
Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.
Related Articles
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


0 Responses to “NISAIDIENI JAMANI MUME WANGU ANANITESA NAONA AIBU HATA KUTOKA NJE YA NYUMBA YANGU ”
Post a Comment
Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.