Monday, July 15, 2013
RAY C ANENEPA GHAFLA, MASHABIKI WA BONGO FLEVA WAMSHANGAA
Monday, July 15, 2013 by Unknown
Mwanamuziki staa wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ ambaye amepotea katika anga la muziki kwa kipindi kirefu kutokana na matatizo ya matumizi ya madawa ya kulevya, amejitokeza akiwa amefutuka.
Hivi karibuni, Ray C ameibuka na kuanza kutundika picha na vipande vya video zake katika kurasa zake kwenye mitandao ya kijamii, ikiwa ni sehemu ya kujiweka karibu na mashabiki wake.
Kufuatia ishu hiyo, kumeibuka mshtuko mkubwa kwa baadhi ya watu kutokana na picha hizo kumuonesha ‘bidada’ akiwa amenenepeana ghafla tofauti na alivyozoeleka.
UNENE UNATOKANA NA DOZI?
Baadhi ya mashabiki wake katika mtandao wa Instagram walidai kuwa inawezekana unene huo unatokana na dozi ya kuacha ‘unga’.
Hata hivyo, wengine walimshukuru Mungu kwa kuwa sasa afya ya mwanadada huyo inaonekana kurudi katika hali yake ya kawaida tofauti na miezi kadhaa aliporipotiwa na gazeti hili akiwa amezimika kutokana na matumizi ya unga.
Katika picha hizo, Ray C anaonekana kufutuka usoni, kifuani na mapajani ambapo awali kabla ya matatizo hakuwa hivyo.
Wengi walimshukuru Mungu kumuona tena Ray C akiwa mzima pamoja na ukimya wake katika muziki.
Ray C amekuwa akitundika picha hizo kwa ajili ya mashabiki na marafiki hasa kupitia Instagram akiambatanisha na maelezo huku nyingine zikizungumza zenyewe.
HATAKI KUTAJA ANAPOISHI
Maelezo ya picha hizo yamekuwa yakielezea maisha ya Ray C kwa sasa akiwa kwenye mjengo wa maana bila kutaja ni sehemu gani.
Kwa mujibu wa mashabiki wa Ray C, mwanadada huyo kwa sasa anakula bata tu huku akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye anamuita ‘Daddy’ kwa kuwa ndiye aliyemsaidia kimatibabu.
Daktari mmoja maarufu jijini Dar aliyehojiwa , alibainisha kuwa kinachosemwa na mashabiki wa Ray C kwamba kinachomnenepesha ni dozi ya kuacha madawa ya kulevya, kinaweza kuwa kweli au kisiwe kweli.
Aliongeza kuwa kunenepa kunachangiwa na vitu vingi kama kupata maisha mazuri yasiyohusisha msongo wa mawazo au mihangaiko ya hapa na pale hivyo anachofanya ni kula, kulala na kustarehe tu.
GPL
Tags:
celebrities ,
udaku

This post was written by: Author Name
Author description goes here. Author description goes here. Follow him on Twitter
Get Updates
Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.
Related Articles
- KAULI ZA MJINI WANASEMA MICHEPUKO SIO DEAL, KWANINI UIBE MKE WA MTU?? TULIA NA WAKO, CHECK HUYU ALIVO UMBUKA NA KUAIBIKA BAADA YA FUMANIZ....
- KUTANA NA MREMBO MWANACHUO MWENYE KALIO LA AJA AMBAYE, WATU WANAHISI ANALITUMIA KUFAHURU MITIHANI
- DUNIA INA MAMBO...ETI AUNT EZEKIEL ACHIZIKA KUPITA MAELEZO..KISA..BUSU LA MBWA...!!
- KUNUKA KIKWAPA NA WEUSI KATIKATI YA MAPAJA YANGU VINANINYIMA RAHA
- FICHUA MAOVU TUNAENDELEZA::FACEBOOK YAINGILIWA NA MAKAHABA:CHEKI PICHA HAPA, JE NI SAWA KWA MADADA ZETU WANACHOKIFANYA FACEBOOK
- TAZAMA PICHA 11 KUTOKA NYUMBANI KWA MAREHEMU MZEE GURUMO DAR USIKU HUU.
- OOOH NOO....POMBE SI CHAI...MASKINI MR NICE ACHEZEA KICHAPO CHA AIBUU BAADA YA KUMSARANDIA DEMU WA WATU...! HABARI KAMILI SOMA NA TAZAMA PCHAZ HAPA
- HATIMAE LUPITA AONYESHA CHUP ALIYOVAA WAKATI AKIPOKEA TUZO YA OSCARS, TAZAMA PICHA HAPA
- UTATA MTUPU...LADY JAY DEE ASEMAMAZITO HAYA: MIMI NA GARDNER TUNAISHI KAMA KAKA NA DADA...!SOMA ZAIDI HAPA...
- WOLPER GAMBE NA PENNY WAPIGA PICHAZ ZA MSHTUKO NA UTATA, KANA KWAMBA NI WATU WALIO JI KWICHI KWICHI WAO KWA WAO,,,YAANI NI KIMAHABA ZAID...JIONEE HAPA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “RAY C ANENEPA GHAFLA, MASHABIKI WA BONGO FLEVA WAMSHANGAA ”
Post a Comment
Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.