Tuesday, July 9, 2013
UGOMVI WA NDOA WASABABISHA MWANAMKE AVAMIWE NA KUKATWA MIKONO YAKE
Tuesday, July 9, 2013 by Unknown
Mwanamke mmoja Sumayi Girandi mkazi wa kijiji cha Kunzugu wilayani Bunda amepoteza vidole vitatu vya mkono wa kulia na kiganja cha mkono wa kushoto kukatwa baada kushambuliwa kwa mapanga na watu wasiojulikana kisa kikidaiwa kuwa kutaka kunyang’anywa mali zake.
Uhodari wa mama huyo wa kutafuta mafanikio ya familia yake hasa baada ya kutengana na mume wake umeishia hapo baada ya watu wasiojulikana kumvamia nyumbani kwake na kumshambulia kwa mapanga na kisha wakamkata kiganja cha mkono wa kushoto na kuanguka.
Kwa sasa Sumayi Girandi anatibiwa katika Hospitali teule ya wilaya.
Vitendo vya kujeruhi na kuua wanawake mkoani Mara kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo ya ndugu kutaka kuwanyang’anya bado vinaendelea.
Katika tukio lingine wilayani Bunda dereva mmoja wa pikipiki ameuawa na watu wasiojulikana ambapo taarifa zinasema kuwa kabla ya kuuawa kwa dereva huyo wa bodaboda inadaiwa alikodiwa na watu wawili.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mara Ferdinand Mtui amethibitisha kutokea kwa matukio hayo na tayari watu wanne wamekamatwa wakiwemo watu wanaotuhumiwa kumkatakata mapanga mwanamke Sumayi Girandi.
Emmanuel Amas, TBC Mara.
Tags:
kitaifa ,
mapenzi

This post was written by: Author Name
Author description goes here. Author description goes here. Follow him on Twitter
Get Updates
Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.
Related Articles
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “UGOMVI WA NDOA WASABABISHA MWANAMKE AVAMIWE NA KUKATWA MIKONO YAKE ”
Post a Comment
Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.