Saturday, July 13, 2013

Ushuduhuda: Upungufu wa Nguvu za Kiume - Tiba Halisi







Mwaka jana nilipost humu jamvini thread kuomba msaada wa tiba ya nguvu za kiume. Kwa kweli ni tatizo lililonisumbua kwa muda mrefu. Sikuwa naweza hata kusimamisha kwa dakika. Kabla ya kuja jamvini nilikuwa nimetembea kwa waganga wengi mnoooo. Nilikula dawa zao za kutosha. Nilienda Mwanza, Arusha, Mbeya, Kenya, DSM, Dom na kwingine kwengi tu. Sikupata hata nafuu kidogo. Nilipokuja humu jamvini nilipata ushauri na hata waganga wengine walinialika nitumie dawa zao kwa kunihakikishia kuwa ni tiba sahihi kwa 100%. Sitawataja kwa sababu ya maadili na kwa kuwa wako kazini na kwa kuwa nimekujatoa ushuhuda. Ukweli ni kuwa nimenunua hizi dawa za hawa waganga nyingine kwa Tshs, USD, rand n.k na nilizitumia kwa uaminifu mkuwa kabisa. Tofauti na nilivofikiri kwa kweli ckupata nafuu hata kidogo.

Kuna jamaa mmoja alinitonya kuwa nenda hispital umwone Dr wa hiyo issue yako. Niliamua kwenda MNH ingawa kwa aibu kubwa mnooo. Wakati najieleza Dr alikatisha maelezo yangu akaniuliza km nna sukari, pumu, k/kikuu nk. Nikamwambia hapana, tatizo langu ni hili hapa. Akaniambia kapime hivi haafu ulete majibu, ckujua ninini. Nilienda kwa vipimo nikachukuliwa damu baada ya muda nikapewa majibu na nikauliza walipima nn. Mtaalamu wa vipimo akaniambia alipima hormones mwilini bac nikarudi kwa dr. Dr baada ya kupitia majibu akaniambia hormones za kiume (testosterone) zimeshuka. Nikamwambia sasa? Akajibu zipandishe. Akaniandikia dawa za miezi mitatu. Kwa kweli nilitumia dawa kuanzia mwezi August 2012 na kufikia september mambo yalianza kubadilika kabisa na mpaka sasa natoa ushuhuda mm ni mwingine kabisa. Sasa nazingatia mlo na mazoezi (gym).

Ushauri wangu kwa wengi wenye hii issue ni kuwa nendeni hospital mkajue ni nni hasa tatizo ndo muanze tiba. Najua Waganga wa humu JF hamtaipenda hii lakini tukubali ukweli, ili watu wasipoteze muda na pesa nyingi km mm nilivofanya. 

Yeyote anaetaka maelezo zaidi an-PM.

Tags:

0 Responses to “Ushuduhuda: Upungufu wa Nguvu za Kiume - Tiba Halisi ”

Post a Comment

Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.

HHHHHHHHHHHH

Subscribe

Kwa habari na Taarifa weka Email yako Hapa tutakutumia

© 2014 FUNUNU HABARI.. All rights reserved.
Designed by FUNUNU HABARI