Home
» celebrities
» JOKATE ATAJA SABABU ZINAZOWAFANYA WANAUME WENGI WAMMEZEE MATE NA KUMTONGOZA KILA SIKU...
Friday, September 13, 2013
JOKATE ATAJA SABABU ZINAZOWAFANYA WANAUME WENGI WAMMEZEE MATE NA KUMTONGOZA KILA SIKU...
Friday, September 13, 2013 by Unknown
MREMBO anayefanya vizuri katika mambo mengi nchini, Jokate Urban Mwegelo (pichani) ametaja sababu nne zinazowafanya wanaume kumzimikia, akiwemo nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Akiandika katika mtandao wake wa Kidoti Life Style, Jokate, mshindi wa pili wa Miss Tanzania 2006, alizitaja sababu hizo kuwa ni kujiamini, kujitegemea, kupendeza na tabasamu muda wote.
“Kujiamini ndiyo sababu kubwa ya kwanza inayonifanya nipendwe zaidi, hamna kitu kinachowavutia watu hasa wanaume kama kujiamini,” anaandika Jokate.
“Kujitegemea ni sababu ya pili, binafsi naamini kwamba hakuna kitu kinachowaboa wanaume kama mwanamke ambaye anapenda vitu vya kupewa. Ukimuonesha mwanaume wewe unapenda kutafuta vyako, basi jua atakupenda zaidi.”
Jokate alisema sababu nyingine inayomfanya kuwa kivutio kwa wanaume ni kupendeza katika mavazi, hasa kwa kuvaa nguo zenye rangi ya kuonekana.
Sababu nyingine aliyoitoa ni tabasamu, akiweka wazi kuwa tabasamu linamfanya aonekane mrembo zaidi.
Read more: http://searchbongo.blogspot.com/2013/09/jokate-aataja-sababu-zinazowafanya.html#ixzz2elZFkWe0
Tags:
celebrities

This post was written by: Author Name
Author description goes here. Author description goes here. Follow him on Twitter
Get Updates
Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.
Related Articles
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “JOKATE ATAJA SABABU ZINAZOWAFANYA WANAUME WENGI WAMMEZEE MATE NA KUMTONGOZA KILA SIKU...”
Post a Comment
Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.