Monday, September 30, 2013

MAJAMBAZI WAVAMIA BENK JIJINI DAR ES SALAAM NA KUPORA ZAIDI YA MILIONI 150



Majambazi saba akiwemo mmoja ambaye amevalia sare za polisi wameiteka benki ya I&M jijini Dar es Salaam na kuchukuwa fedha zinazohisiwa kuwa ni zaidi ya shilingi milioni 150 na kutokemea kusikojulikana.

Tukio hilo limetokea katika benki hiyo iliyoopo katika makutano ya mtaa wa Indira Gandi na Mosque ambapo baadhi ya mashuhuda wameelezea tukio hilo lilivyokuwa.


Akizungumza katika eneo la tukio kamanda wa polisi mkoa wa Ilala kamanda Marieta Minagi amesema bado wanaendelea kufanya uchunguzi wa tukio lenyewe ingawa mpaka sasa ni kama milioni zaidi 150 zinahisiwa kuibiwa.


Naye mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Said Meki Sadiki akiwa katika eneo hilo amesema matukio ya Kuiba fedha katika benki yanazidi kushamiri na hivyo kuna haja ya taasisi husika kujipanga upya.

Hata hivyo ITV ilishuhudia baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo wakipandishwa katika gari la polisi lenye namba za usajili T220 AMV na kuondoka nao kwa ajili ya mahojiano zaidi.

Tags:

0 Responses to “MAJAMBAZI WAVAMIA BENK JIJINI DAR ES SALAAM NA KUPORA ZAIDI YA MILIONI 150”

Post a Comment

Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.

HHHHHHHHHHHH

Subscribe

Kwa habari na Taarifa weka Email yako Hapa tutakutumia

© 2014 FUNUNU HABARI.. All rights reserved.
Designed by FUNUNU HABARI