Thursday, September 12, 2013

Mwandishi wa gazeti la MWANANCHI akatwa katwa mapanga mkoani SINGIDA




Mwandishi wa habari wa gazeti la The Citizen na mwananchi mkoani Singida, Awila Silla amenusurika kuuawa na mtu anayedhaniwa kuwa Jambazi baada ya kukatwa katwa mapanga kichwani na kusababisha kuzirai. Tukio hilo limetokea juzi saa mbili usiku jirani na mahakama ya mwanzo ya Utemini mjini Singida. 
Awila ambaye amelazwa wodi 2 katika hospitali ya mkoa amedai kuwa baada ya kukutana na kijana huyo aliamuriwa kutoa fedha na baada ya kudai hana, jibu hilo lilisababisha kijana huyo kuanza kumkata Mapanga na alipoangauka na kuzirai alinyang’anywa simu yake ya kiganjani .
Hata hivyo Awila amedai kuwa bado hajatoa taarifa ya tukio hilo polisi

Tags:

0 Responses to “Mwandishi wa gazeti la MWANANCHI akatwa katwa mapanga mkoani SINGIDA”

Post a Comment

Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.

HHHHHHHHHHHH

Subscribe

Kwa habari na Taarifa weka Email yako Hapa tutakutumia

© 2014 FUNUNU HABARI.. All rights reserved.
Designed by FUNUNU HABARI