Home
» burudani
» TAZAMA PICHA 100 ZA SHOW NZIMA YA P-SQUARE ILIVYOFUNIKA MBAYA USIKU WA KUAMKIA LEO
Saturday, November 23, 2013
TAZAMA PICHA 100 ZA SHOW NZIMA YA P-SQUARE ILIVYOFUNIKA MBAYA USIKU WA KUAMKIA LEO
Saturday, November 23, 2013 by Unknown
Jumamosi hii, P-Square wamefanikiwa kudhihirisha kwanini wao ni namba
moja Afrika na wanastahili kuwa kundi la muziki linalolipwa fedha
nyingi zaidi, baada ya kuzikonga nyoyo za mashabiki wa Dar es Salaam kwa
show kali, yenye nguvu, ya kutikisa na ndefu kwenye viwanja vya Leaders
Club.

Paul akipanda stejini
P-Square ambao walisindikizwa na bendi yenye watu wanne tu (mpiga
drums, mpiga kinanda, mpiga gitaa la bass na gitaa la solo), walitoa
mfano wa namna live show inavyotakiwa kufanywa. Wakitaniana mara kwa
mara jukwaani na kuendesha mashindano ya wao kwa wao, Peter na Paul
Okoye walipiga show ya takriban masaa matatu, kwa kasi, nguvu na uwezo
ule ule, kuanzia mwanzo hadi mwisho.

Peter akiimba wimbo kwa hisia kali
Ilikuwa ni mpaka usikilize kwa makini kutofautisha kile bendi hiyo na
wao walivyokuwa wakiimba na wimbo uliorekodiwa, kwakuwa bendi hiyo kali
inayojua muziki ilipiga nyimbo zao kwa ustadi mkubwa.

Paul akiimba kwa hisia pia
P-Square waliimba karibu nyimbo zote zao zilizotamba na kuufanya
umati mkubwa uliojitokeza Leaders upige kelele muda wote na kuimba nao
nyimbo hizo. Kwa maneno yao wenyewe, P-Square wamesema show ya Dar
ambayo iliandaliwa na East Africa Radio na kudhaminiwa na Vodacom,
ilikuwa ya kuvutia kuliko zote walizowahi kufanya Afrika Mashariki.
Pamoja na nyimbo zao, pia waliimba nyimbo za wasanii wengine kama Usher, 2face, Radio n Weasel na wengine.

Mpiga gitaa wa P-Square
Awali kabla ya P-Square, Ben Pol, Lady Jaydee na Joh Makini pamoja na
Weusi walitangulia kwa show zilizoshangiliwa kwa kiasi kikubwa pia. Kwa
ufupim show ya P-Square imefanikiwa sana.
Miongoni mwa matukio yaliyotia fora ni pamoja na mrembo huyo chini
kupandishwa jukwaani na kupewa cheo (kwa utani) cha mke wa pili wa Peter
aliyefunga ndoa juzi jijini Lago.

Mrembo aliyepandishwa jukwaani na P-Square kutambulishwa kama Onyinye wa Tanzania


Peter amkibusu mrembo huyo

Onyinye akivishwa saa na Peter















Paul akivuta hisia

Paul akiwajibika jukwaani

Paul Okoye

Peter akimsikiliza kaka yake Paul

Peter akitafakari kitu

Peter akiuangalia kwa tabasamu umati mkubwa uliojitokeza Leaders Club

Peter akiwa haamini umati mkubwa uliojitokeza Leaders

Peter mara baada ya kubaki kifua wazi

Peter mara baadaya kuvua nguo ya juu

Profesa Jay

Waimbaji wa Machozi Band

Weusi wakiwa stejini

Ben Pol akisindikizwa na bendi ya Machozi akitoa burudani

Ben Pol akitumbuiza

Joh Makini

Lady akiwa ndani ya mavazi kama ya askari wa kike

Lady Jaydee pamoja na Machozi Band akitumbuiza

MC wa pili wa shughuli, T-bWAY

MC wa shughuli, Dulla akisherehesha

Mpiga gitaa wa P-Square

Nikki wa Pili baada ya kupanda kumpa shavu kaka yake Joh Makini

Nikki wa Pili





















Beautiful Onyinye wa Tanzania aliyechaguliwa na P-Square

Esi, Jokate na Martin Kadinda

Faiza akifurahia burudani

Faiza wa EATV akichukua picha

Jokate Mwegelo

Mashabiki wa burudani wakifurahia bia wakati burudani ikiendelea

Mrembo wa kizungu akiangalia shughuli ya P-Square

Mrembo wa mwenye nguo nyeupe alitia fora baada ya kuitwa
jukwaani na Peter na kupewa heshima ya kuwa Beautiful Onyinye wa
Tanzania

Mzungu huyu aliyejichora tatto mwili mzima aliamua kusogea karibu pia kuwashuhudia P-Square

Ni furahaa tu

Rihanna wa Bongo akijimwaya na burudani ya mapacha hao wa Nigeria

Rihanna wa Bongo

Shabiki wa P-Square akiwa ameshika bango lenye ujumbe maalum kwa mapacha hao

Show ilihudhuriwa na watu wa mataifa mbalimbali

Wapenzi wakidokezana jambo

Warembo wakifurahia mbele ya camera ya Bongo5

Zari aka The Boss Lady wa Uganda akichukua picha za P-Square

Zari aliamua kusafiri kutoka Kampala, Uganda kuja kuwashuhudia P-Square

























Source: Bongo5
Tags:
burudani

This post was written by: Author Name
Author description goes here. Author description goes here. Follow him on Twitter
Get Updates
Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.
Related Articles
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “TAZAMA PICHA 100 ZA SHOW NZIMA YA P-SQUARE ILIVYOFUNIKA MBAYA USIKU WA KUAMKIA LEO”
Post a Comment
Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.