Tuesday, March 19, 2013
AFRICAN BARRICK GOLD KUONGEZA UWEKEZAJI WA MFUKO WAKE WA MAENDELEO WA ABG
Tuesday, March 19, 2013 by Unknown



……………………………………………………………………………………
• Zaidi ya miradi 50 yapatafa ufadhili wa Mfuko wa Maendeleo wa kampuni ya ABG
• ABG yasisitiza kuendelea kuwekeza dola za Marekani milioni 10 kwenye mfuko
Kampuni ya uchimbaji madini ya African Barrick Gold (ABG) inafuraha kutoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Mfuko wa Maendeleo wa ABG tangu kuanzishwa kwake mnamo Septemba 2011.
Mfuko huu umesimamia uwekezaji wa kampuni ya ABG kwenye jamii katika kipindi kilichopita cha miezi 18 na kufanikiwa kutekeleza zaidi ya miradi 50 yenye thamani ya dola za Marekani milioni 7.5 (takriban shilingi bilioni 12 katika kipindi cha mwaka 2011/12.
Greg Hawkins, Afisa Mtendaji Mkuu wa ABG, amesema: “Tunafurahi kuona mafanikio makubwa ambayo Mfuko wa Maendeleo wa ABG umeyapata kwenye kipindi cha miezi 18 mpaka sasa. Tulianzisha Mfuko huu kama sehemu ya jitihada zetu za kuchangia kwenye maendeleo endelevu nchini Tanzania na tayari tumeona mafanikio makubwa kwenye zaidi ya miradi 50 mpaka sasa.”
”Tunaendelea kuweka msisitizo kuhakikisha kuwa jamii zinazotuzunguka zinapata faida kutokana na kuwepo wa shughuli zetu kwenye maeneo yao na ninafurahi kutangaza kuwa kampuni ya ABG itaendelea kutenga dola za Marekani milioni 10 kila mwaka kwa ajili ya uwekezaji wa Mfuko wa Maendeleo wa ABG kwa mwaka 2013.”
Mpaka hii leo, Mfuko wa Maendeleo wa ABG umewekeza dola za Marekani milioni 2.2 (zaidi ya shilingi bilioni 3.6) kusaidia kuboresha afya ya umma kwenye jamii zinazozunguko migodi yake.

This post was written by: Author Name
Author description goes here. Author description goes here. Follow him on Twitter
Get Updates
Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.
Related Articles
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “AFRICAN BARRICK GOLD KUONGEZA UWEKEZAJI WA MFUKO WAKE WA MAENDELEO WA ABG ”
Post a Comment
Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.