Thursday, March 21, 2013

HAYA NI MAELEZO YA SHAHIDI KUHUSU TUKIO LA KUTISHA LA DEREVA KUPIGWA RISASI KTK FOLENI KINONDONI




.

Mpaka sasa hivi sijapata maelezo yoyote kutoka kwa Polisi Kinondoni kuhusu kijana alieuwawa kwa risasi akiwa anaendesha gari dogo kwenye foleni Kinondoni Dar es salaam march 20 2013.

Nafasi hii naitumia kumkariri mmoja wa mashuhuda wa hilo tukio akisema “ni kwenye barabara ya kutoka Magomeni kwenda Mkwajuni hii gari ilikua inashuka, kwa sababu sasa hivi kuna foleni upande wa kulia kuna magari upande wa kushoto kuna magari, pikipiki kama kawaida zikawa zinatanua katikati”

“Wakati pikipiki ya muhusika ilipotanua ghafla ilibidi dereva huyu aliyeuwawa amkwepe hivyo akagonga gari lake kwenye kingo za barabara na kupasua tairi, marehemu akatoka kwenye gari na kukutana na jamaa wa pikipiki wenye asili ya kiarabu wakaanza kubishana na kuwaambia amepasua tairi kwa sababu alikua anawakwepa wao kwa hiyo wamlipe tairi lake tu” – Shuhuda

“Wale waarabu walikua na waya flani kama za shoti, yani zinapiga shoti ndio wakawa wanawapiga kama shoti mwilini.. zikatokea purukushani Mwarabu mmoja akamwambia Marehemu nitakuua, yule Marehemu akasema huna uwezo wa kuniua wewe… ndio mwarabu akampiga risasi ya shingo na kudondoka palepale na kufariki, majirani ndio wakachukua kanga na kumfunika, mpaka naondoka pale Polisi walikua wamefika kwenye eneo la tukio” – Shuhuda

Bado naendelea kuisubiri kauli ya polisi kuhusu hili tukio, pia nina ahadi ya kukutana na mmoja kati ya vijana waliokua pamoja na marehemu kwenye gari wakitokea gereji

CREDIT - MILAD AYO


Tags: ,

0 Responses to “HAYA NI MAELEZO YA SHAHIDI KUHUSU TUKIO LA KUTISHA LA DEREVA KUPIGWA RISASI KTK FOLENI KINONDONI ”

Post a Comment

Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.

HHHHHHHHHHHH

Subscribe

Kwa habari na Taarifa weka Email yako Hapa tutakutumia

© 2014 FUNUNU HABARI.. All rights reserved.
Designed by FUNUNU HABARI