Home
» kitaifa
» Mstahiki Jerry Silaa amtembelea mtoto wa kwanza kuzaliwa katika Zahanati ya G/Kwalala aliyoijenga 2007-2010.
Wednesday, March 20, 2013
Mstahiki Jerry Silaa amtembelea mtoto wa kwanza kuzaliwa katika Zahanati ya G/Kwalala aliyoijenga 2007-2010.
Wednesday, March 20, 2013 by Unknown

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi katika Zahanati ya Guluka Kwalala iliyopo katika Halmashauri yake baada ya kuwasili kwa ajili ya kumpongeza Mkazi wa eneo hilo kwa kujifungua Salama mtoto wa Kwanza katika Wodi ya Wazazi aliyoijenga kwa nguvu zake kwa ajili ya wakazi wa eneo hilo ikiwa ni kutekeleza katika moja ya ahadi alizozitoa kwa wapiga kura wake.

Mstahiki Meya Jerry Silaa akimsalimia na kumpongeza Bi. Halima Abubakari aliyejifungua mtoto wake katika Zahanati G/Kwalala iliyojengwa na Mstahiki Meya.

Mstahiki Meya Jerry Silaa akiwa amepakata mtoto wa Bi. Halima Abubakary mkazi wa Kata ya Gongo la Mboto katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala aliyejifungua salama usiku wa kuamkia Machi 19, 2013 kwenye Zahanati iliyojengwa na Mstahiki Meya ikiwa ni kutekeleza ahadi zake kwa wapiga kura wake.

Mstahiki Meya Jerry Silaa akimchekesha mtoto huku akiwa ameshikilia zawadi ya mtoto kwanza kuzaliwa kwenye Zahanati yake.

Mstahiki Meya Jerry Silaa akisaini kitabu cha wageni katika wodi ya wazazi iliyopo kwenye Zahanati ya G/Kwalala.

Mstahiki Meya Jerry Silaa akipongezwa na baadhi ya wakazi wa eneo hilo kwa kuwasogezea huduma za Afya karibu na makazi yao.

Tangazo la kutoa huduma ya kujifungua lililobandikwa nje ya Zahanati hiyo.

Bango la Zahanti ya Guluka Kwalala iliyojengwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa.
--
Zahanati ya G/Kwalala imejengwa mwaka 2007-2010 na Mh. Jerry Silaa. Mwaka 2012 alijenga wodi ya kinamama kujifungua na kuaznia mwezi Februari 2013 iliwekwa vifaa vyote vinavyohitajika na aliahidi zawadi kwa mtiti wa kwanza ambaye amezaliwa usiku wa kuamkia tarehe 19 Machi, 2013.
Tags:
kitaifa

This post was written by: Author Name
Author description goes here. Author description goes here. Follow him on Twitter
Get Updates
Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.
Related Articles
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “Mstahiki Jerry Silaa amtembelea mtoto wa kwanza kuzaliwa katika Zahanati ya G/Kwalala aliyoijenga 2007-2010. ”
Post a Comment
Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.