Thursday, May 2, 2013
ALONSO MCHEZAJI WA KWANZA KUSAJILIWA NA MOURINHO CHELSEA.
Thursday, May 2, 2013 by Unknown
KOCHA Jose Mourinho yuko tayari kumfanya Xabi Alonso awe mchezaji wa kwanza kusajiliwa atakaporejea Stamford Bridge mwishoni mwa msimu kuifundisha tena Chelsea.
Kocha huyo wa Real Madrid alihusishwa kwa kiasi kikubwa na kurejea Chelsea baada ya timu yake kutolewa katika Ligi ya Mabingwa Ulaya akihama Bernabeu mwishoni mwa msimu.
Kocha huyo wa Kireno mwenye umri wa miaka 50 alisema atakwenda sehemu ambayo anapendwa, vyombo vingi vya habari vikisema Magharibi mwa London, ambako aliifundisha Chelsea akiibebesha mataji matatu kabla ya kuondoka mwaka 2007 ndiko anakopendwa zaidi.
Huku kuelekea Chelsea: Jose Mourinho atahamia na Xabi Alonso na London

Unaondoka Jose? Alonso (kulia) inaaminika yuko kwenye mipango ya Mourinho, akihamia Chelsea mwishoni mwa msimu
Inafahamika kwamba Mourinho tayari amemtambulisha nyota huyo wa zamani wa Liverpool kama mmoja wa wachezaji atakaowasajili ikiwa atakwedna kurithi mikoba ya Rafa Benitez.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 31 wa kimataifa wa Hispania, ambaye alitwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya na Liverpool mwaka 2005, atamaliza mkataba wake msimu ujao na bado hajakubali ofa ya nyongeza ya mkataba wa miaka kuendelea kuishi Madrid.
Kwa mujibu wa gazeti la Independent, Alonso ni mmoja kati ya marafiki wa karibu wa Mourinho ndani ya Real na amesitisha uamuzi wake hadi ajue nani atarithi mikoba ya Mreno huyo.
Akihamia Chelsea, dhahiri atawaumiza mashabiki wa Liverpool, kwani aliwahi kusema atakaribisha ofa ya kurejea Anfield.
Wazi pia akihamia Stamford Bridge itakuwa utata kati yake na kiungo wa England, ambaye pia ni swahiba wa Mourinho, Frank Lampard aliyekubali kuongeza mkataba wa mwaka mmoja.
Mshambuliaji wa Atletico Madrid, Rademel Falcao, waakti huo huo inaaminika ni mchezaji anayetakiwa zaidi The Blues, ingawa kuna mchuano mkali na klabu nyingine, Manchester United na Manchester City kuwania saini ya Mcolombia huyo.
Tags:
michezo

This post was written by: Author Name
Author description goes here. Author description goes here. Follow him on Twitter
Get Updates
Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.
Related Articles
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ALONSO MCHEZAJI WA KWANZA KUSAJILIWA NA MOURINHO CHELSEA. ”
Post a Comment
Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.