Thursday, May 2, 2013
MHINDI ALIYEMUUA MWALIMU ELIZABETH NAYE AKUTWA AMEJIUA GESTI
Thursday, May 2, 2013 by Unknown
MHINDI mwenye uraia wa India, Srinivasa Rao Talluri, 36 anayedaiwa kumuua Mwalimu Elizabeth Mmbaga wa Shule ya Msingi Atlas, jijini Dar es Salaam amejiua Aprili 17 mwaka huu katika Hoteli yaTransit iliyopo Karakata.
Talluri ambaye alikuwa akifanya kazi katika kampuni ya vinywaji vikali ijulikanayo kwa jina la Moan’s Drinks Ltd iliyopo Oysterbay, Dar maiti yake ilikutwa chumbani saa mbili asubuhi na inadaiwa alijiua kwa kunywa sumu ambayo mabaki yake yamepelekwa Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa uchunguzi. Habari za kipolisi zimesema kuwa baada ya wafanyakazi wa Hoteli ya Transit jijini Dar kugundua kuwa Mhindi huyo amekufa, walitoa taarifa polisi ambao walifika na walipochunguza chumbani, walikuta kuna pombe aina ya Pushkin chupa tatu, chupa yenye sumu ya kuulia wadudu, chips na maziwa glasi moja.
Inadaiwa kwamba Mhindi huyo aliachishwa kazi katika kampuni hiyo Aprili 2, mwaka huu baada ya kugundulika kuwa alitumia vibaya zaidi ya shilingi 400,000 ambapo Aprili 3, mwaka huu alifikishwa polisi Kituo cha Oysterbay, jijini Dar. Mwandishi wetu alifika katika ofisi za Moan’s Drinks Ltd alikokuwa akifanyia kazi Mhindi huyo na kuonana na mmoja wa viongozi wa kampuni hiyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Raju na akakiri kutokea kwa kifo cha Talluri. Habari zinasema mwili wake ulifanyiwa uchunguzi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Jumatatu iliyopita na ukasafirishwa kupelekwa India Jumatano ya wiki iliyopita kwa ajili ya mazishi.
CREDIT-joycekiria.com
Tags:
mapenzi

This post was written by: Author Name
Author description goes here. Author description goes here. Follow him on Twitter
Get Updates
Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.
Related Articles
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MHINDI ALIYEMUUA MWALIMU ELIZABETH NAYE AKUTWA AMEJIUA GESTI ”
Post a Comment
Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.