Monday, June 17, 2013
Mama Kanumba, Mama Lulu Wageuka Kituko Kwa Ujio Wa Kanumba Mpya
Monday, June 17, 2013 by Unknown
MAMA wa marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa na mama wa mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’, Lucresia Karugila wamegeuka kituko baada ya kunaswa wakishangilia kumpata ‘Kanumba mpya’.
Tukio hilo ambalo liliwafanya watu wengi wapigwe na butwaa, lilitokea hivi karibuni katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo wamama hao ambao watu hawakudhania kama ni mashosti, walisikika wakipiga shangwe wakisema wamepata mtoto wa kiume kupitia kwa mtoto wa mama Kanumba aitwaye Adela kisha kumfananisha na marehemu Kanumba.
Mwandishi wetu ambaye alikuwepo eneo hilo, alipowauliza kulikoni wapige kelele nyingi za shangwe, mama Kanumba ndiye alikuwa wa kwanza kuzungumza:
“Tuna furaha sana kuzaliwa kwa Kanumba The Great leo, tulikuwa tukimsubiri kwa hamu sana na hatimaye leo amezaliwa.”
Wakati mama Kanumba alipokuwa akimalizia kuzungumza, mama Lulu naye akadakia:
“Kipindi chote tulikuwa tukiomba sana tumpate mtoto wa kiume na tulikuwa tumepanga tumpe jina la Kanumba kwa hivyo hapa tuna furaha kumpata Kanumba mpya.”
Mama Kanumba na mama Lulu kwa sasa wanadaiwa kuwa ni marafiki wa kutupwa na mara nyingi wamekuwa wakinaswa katika viwanja tofauti vya starehe jijini.TOA MAONI YAKO HAPA
Tags:
celebrities ,
udaku

This post was written by: Author Name
Author description goes here. Author description goes here. Follow him on Twitter
Get Updates
Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.
Related Articles
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “Mama Kanumba, Mama Lulu Wageuka Kituko Kwa Ujio Wa Kanumba Mpya”
Post a Comment
Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.