Friday, July 12, 2013

DIDA APIGWA DONGO"TULIA SASA NA HIYO NDOA TUMECHOKA KUHUDHURUA SHEREHE ZA NDOA ZAKO"



BAADA ya hivi karibuni Mtangazaji wa Radio Times, Khadija Shaibu ‘Dida’ kufunga ndoa na mwanaume aitwaye Ezden, mashosti zake wamemtaka kutulia sasa na asijaribu kugeuza ndoa kuwa fasheni. Wakizungumza na Ijumaa kwa nyakati tofauti, baadhi ya mastaa walioomba hifadhi ya majina yao ambao walihudhuria ndoa hiyo iliyofungwa Ijumaa iliyopita Ubungo jijini Dar walisema, wamechoka na mialiko ya ndoa zake kila baada ya kipindi kifupi hivyo ni wakati sasa wa kutulia, Hii ni ndoa ya Tatu ya Dida.


“Asifanye ndoa kama fasheni, tumechoka kuhudhuria sherehe za ndoa yake, kama ana kasoro, ajirekebishe ili atulie sasa ajenge maisha yake,” alisema staa mmoja ambaye ni rafiki wa karibu na ndugu wa Dida. Hata hivyo, akizungumzia kuhusu kuolewa huko, Dida alisema safari hii ndoa yake ikivunjika haolewi tena.



Kwa hisani ya Na Hamida Hassan /GPL

Tags: ,

0 Responses to “DIDA APIGWA DONGO"TULIA SASA NA HIYO NDOA TUMECHOKA KUHUDHURUA SHEREHE ZA NDOA ZAKO" ”

Post a Comment

Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.

HHHHHHHHHHHH

Subscribe

Kwa habari na Taarifa weka Email yako Hapa tutakutumia

© 2014 FUNUNU HABARI.. All rights reserved.
Designed by FUNUNU HABARI