Friday, July 12, 2013
JESHI LA POLISI TANZANIA LAAMUA KUMFUATA AGNESS MASOGANGE AFRIKA KUSINI
Friday, July 12, 2013 by Unknown

Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia Dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa aliliambia gazeti hili kwa simu jana kuwa watawapeleka polisi kuwahoji na wanaamini wahusika watawaeleza wahusika wa mzigo huo.
Wasichana hao walikamatwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Oliver Tambo nchini Afrika Kusini wakitokea Tanzania wakiwa na kilo 150 za dawa za kulevya aina ya Crystal Methamphetamine.
“Tutawapeleka askari wetu kuwahoji, tumekwishaanza uchunguzi wa hili...wote watakaohusika katika hili tutawakamata, lakini tunakwenda polepole hatua kwa hatua kuhakikisha tunawanasa wahusika sahihi,”alisema Nzowa.
Naye Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, (JNIA), Moses Malaki alieleza kushangazwa na kiasi kikubwa kupitishwa kwenye uwanja huo licha ya kuwa wapo watu wenye dhamana ya kuangalia usalama.
“Sitaki kusema tutafanya nini, lakini ninachotaka kukwambia ni kwamba uchunguzi umeanza na suala zima tumewaachia polisi na sisi tutatoa ushirikiano kwa kila hatua watakayotutaka, lazima kukomesha hili.
“Tutaangalia nani walikuwa zamu siku hiyo,” alisema Malaki.
Tags:
celebrities ,
udaku

This post was written by: Author Name
Author description goes here. Author description goes here. Follow him on Twitter
Get Updates
Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.
Related Articles
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “JESHI LA POLISI TANZANIA LAAMUA KUMFUATA AGNESS MASOGANGE AFRIKA KUSINI ”
Post a Comment
Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.