Friday, September 13, 2013

MWANAMKE AKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA AKIWA AMEYAFICHA KWENYE MIMBA BANDIA








Kila kukicha vita dhidi ya biashara haramu ya dawa za kulevya inazidi kupamba moto, wakati mataifa mbalimbali yakizidi kuimarisha udhibiti wa biashara hiyo, na wafanyabiashara hiyo wanazidi kuja na mbinu mpya za kusafirisha dawa hizo.


Huko Colombia mwanamke mmoja raia wa Canada amekamatwa uwanja wa ndege akiwa na tumbo la ujauzito wa bandia ambalo ndani yake alificha kilo mbili za dawa za kulevya aina ya Cocaine.


Polisi wa uwanja wa ndege wa Bogota Colombia alimshtukia mwanamke huyo Tabitha Leah Ritchie aliyeonekana kuwa na tumbo lisilo la kawaida ndipo baada ya kumkagua wakakutana na dawa hizo.

Bongo 5

Tags: ,

0 Responses to “MWANAMKE AKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA AKIWA AMEYAFICHA KWENYE MIMBA BANDIA”

Post a Comment

Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.

HHHHHHHHHHHH

Subscribe

Kwa habari na Taarifa weka Email yako Hapa tutakutumia

© 2014 FUNUNU HABARI.. All rights reserved.
Designed by FUNUNU HABARI