Thursday, October 3, 2013

EXCLUSIVE: NIYONZIMA AUNGULIWA NA NYUMBA JIJINI DAR, MAJIRANI WAOKOA FAMILIA YAKE




Kiungo nyota wa Yanga, Haruna Niyonzima ameunguliwa na nyumba yake.




Nyumba anayoishi iko Magomeni jijini Dar es Salaam na moto huo ulianza saa 12 alfajiri hadi ulipozimwa na majirani saa moja asubuhi leo.








Taarifa zinasema nyumba hiyo imeungua kutokana na hitilafu ya umeme katika moja ya nyanya ndani ya nyumba hiyo.


Vitu kadhaa vya thamani ndani ya nyumba yake vimeteketea kwa moto lakini familia yake imesalimika baada ya majirani kuwaokoa.








“Kweli ninawashukuru sana majirani kwa kuonyesha uungwana wa hali ya juu, bila ya wao nyumba yote ingeungua.




“Lakini kuna vitu vichache vimefanikiwa kutoka ila vingi sana vimeungua na moto huo uliokuwa mkali sana,” alisema.


Hadi blogu hii inaondoka eneo la tukio asubuhi hii, baadhi ya watu na mashabiki wa Yanga walikuwa wamefika kwa ajili ya kutoa msaada zaidi.


Pia fundi wa umeme alikuwa anasubiriwa ili kuangalia hitilafu iliyosababisha moto ilitokana na kitu gani.
BY SALEHE JEMBE

Tags:

0 Responses to “EXCLUSIVE: NIYONZIMA AUNGULIWA NA NYUMBA JIJINI DAR, MAJIRANI WAOKOA FAMILIA YAKE”

Post a Comment

Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.

HHHHHHHHHHHH

Subscribe

Kwa habari na Taarifa weka Email yako Hapa tutakutumia

© 2014 FUNUNU HABARI.. All rights reserved.
Designed by FUNUNU HABARI