Home
» burudani
» MFAHAMU VIZURI MCHEZA BRIAN DEACON ALIYECHEZA FILAMU YA JESUS "YESU" MWAKA 1979 NA ANACHOKIFANYA SASA..!!
Tuesday, October 22, 2013
MFAHAMU VIZURI MCHEZA BRIAN DEACON ALIYECHEZA FILAMU YA JESUS "YESU" MWAKA 1979 NA ANACHOKIFANYA SASA..!!
Tuesday, October 22, 2013 by Unknown
Brian
Deacon ndio jina lake mwigizaji huyo ambaye ni mwingereza aliyezaliwa
mnamo tarehe 13/02/1949 huko Oxford nchini Uingereza akiwa ni mtoto wa
pili katika familia yao baba yake akiwa fundi makenika na mama yake
akiwa ni nesi.
Ndoa
yake ya kwanza na Rula Lenska ilivunjika ambapo alizaa na mkewe huyo
binti yao aitwaye Lara Deacon,ndoa yake ya pili alioana na mwanamama
Natalie Bloch mnamo mwaka 1998 mpaka sasa wapo kwenye ndoa hiyo.
Brian Deacon ndani ya filamu ya ''JESUS''
Aliigiza
filamu ya Yesu ambayo pia ilimfanya aokoke mara baada ya kuitazama
akiwa na miaka 30,baada ya kupita kwenye mchujo mkali wa waigizaji zaidi
ya elfu moja ambao walifanyiwa mahojiano huku 260 wakijaribishwa
kuigiza(screen test)kuona kwamba wanafaa akiwa ni mwingereza pekee kati
ya waigizaji Waisrael walioingia kwenye usaili huo akiwa chini ya
kampuni iitwayo New shakespears ambako alikuwa akifanya sanaa za
majukwaani na uigizaji.
Brian Deacon miaka iliyofuatia baada ya kuigiza kama Yesu.
Amesema
kabla ya kuchaguliwa mtihani wake wa kwanza ulikuwa kutoka kwa wakala
wake aliyemvunja moyo kwakumweleza hadhani kama yeye(Brian)atafaa kwenye
kumwigiza Yesu,lakini anasema alifanikiwa,baada ya hapo akawa na wakati
mgumu kutoka kwa watu ambao kila mmoja alikuwa anajaribu kumweleza
jinsi anavyotakiwa kuigiza,sauti yake na mambo mengine,ingawa yeye
alisema nitatumia sauti yangu na maelezo kutoka kwa muongozaji.
Amesema
wiki tatu kabla hawajaanza kurekodi filamu hiyo alisoma kitabu cha Luka
mtakatifu zaidi ya mara 20 kwakuwa filamu hiyo imenukuliwa kutoka
kitabu hicho ambapo Brian amesema kusoma kwake kulimpa nguvu sana na
moyo wa kuigiza filamu hiyo na kuweza kumfahamu vyema Yesu kuwa ni mtu
wa aina gani.
watu wakiangalia filamu ya Yesu ambayo bwana Brian Deacon ni mwigizaji mkuu.
Katika
miezi saba waliyochukua kuigiza filamu hiyo Brian amesema,walikuwa
wanaigiza kwa masaa mengi kuanzia saa kumi za alfajiri mpaka mwisho wa
siku kiasi kwamba wakati mwingine aliwaambia wenzake kwamba wamsaidie
kwani amechoka sana hajui kwamba angeweza kuigiza kwa siku hiyo lakini
anasema alikuwa anashangazwa na nguvu za ajabu alizokuwa akizipata na
kuendelea kuigiza ingawa wakati huo nasema alikuwa mkristo jina wa
kanisa katoliki,alikuwa anauwalakini kuhusu mafundisho na huduma ya Yesu
kwa ujumla,siku moja wakati anaigiza alikuwa anawaombea watu mara
mwanamke mmoja alishika mkono wake kumbe alikuwa na mapepo alimuombea na
mapepo yalimtoka mwanamama huyo.
Siku
nyingine waliokuwa wakiigiza kama wanafunzi wa Yesu wapatao 12 wakiwa
ndani ya basi walikuwa wamepanga kugoma kutokana na malipo waliyokuwa
wakipata cha ajabu Brian anasema director alikuja kumuomba
yeye(Brian)azungumze nao warejee kazini akashangaa akamwambia mimi sio
Yesu ni Brian Deacon,akaamua kuzungumza nao,baada ya masaa 36 walikubali
kurudi kuendelea na kazi
Amesema mtihani mwingine ni siku
alipokuwa hotelini Tel Aviv ghorofa ya 18 usiku mara kukawa na moto
hotelini hapo baada ya mwingereza mmoja aliyekuwa akivuta sigara kusahau
kuizima hivyo kusababisha moto,lakini anasema bahati nzuri hakuna
aliyejeruhiwa ila walifanya kazi siku inayofuatia muda mrefu bila
muongozaji kujali kwamba hawakulala vyema usiku.
watumishi wa Mungu wakiwa njiani kwenda kuonyesha filamu ya Yesu katika uinjilisti huko Kongo.
Amesema
siku hiyo mmoja wa waigizaji anayeitwa Tom Panella alianzisha mada kwa
kusema moto uliokuwa umetokea ni hila za shetani,na kusababisha mjadala
wa muda mrefu ni vipi shetani anahusishwa kwenye swala hilo lakini jibu
likawa,shetani hataki filamu hiyo irekodiwe ndio maana analeta hila
zake.haikuwa kazi rahisi kurekodi filamu hiyo na pia si ujuzi wa
kufurahia,baada ya kumaliza kurekodi kwa takribani miezi 18 ilianza
kuonyeshwa kwa baadhi ya watu na ndipo hata yeye kwa mara ya kwanza
akaona ni kwa jinsi filamu hiyo ilivyonanguvu,ukweli na kugusa mioyo ya
watu
Baada ya filamu hiyo Briana anasema alirudi kuigiza
majukwaani na kwenye runinga, ambapo kwa miaka zaidi ya 30 sasa tangu
kutoka filamu ya Yesu tayari imetazamwa na watu zaidi ya bilioni tatu
katika nchi 233(kwa takwimu za mwaka 2001),zaidi ya watu milioni 117
waliamua kubadilisha maisha yao na kumpokea Yesu,filamu hiyo ambayo
ilitengenezwa chini ya Campus Crusade for crusade ambao kwasasa wanaitwa
Life Ministry pia nchini Tanzania wapo chini ya mkurugenzi Dismas
Shekhalage.ambapo tayari imetafsiriwa katika lugha zaidi 500 huku
nyingine zaidi ya 200 zikiwa njiani kutafsiriwa.
Brian anawaambia
watu kwamba yeye ni mwigizaji tu na sio Yesu kama watu wengine na
kuwataka watu hao kujua hivyo ambapo anasema ameendelea kupata barua
mbalimbali za kumpongeza na kumshukuru kwa kazi nzuri aliyofanya kwenye
filamu hiyo,ambapo kwa upande wake anasema anayo nakala ya filamu hiyo
kwenye maktaba yake nyumbani kwao Uingereza,ambapo kwa takribani miaka
20 filamu hiyo imekuwa ikitazamwa duniani kote na kubadilisha maisha ya
watu.
kati ya filamu alizowahi kushiriki ni pamoja na A zed &
Two Noughts ya mwaka 1985,The Feathered Serpent ya mwaka 1976-1978 na
Tamthilia ya iitwayo Lillie iliyoigizwa mwaka 1978 akitumia jina la
Frank Miles.
Tags:
burudani

This post was written by: Author Name
Author description goes here. Author description goes here. Follow him on Twitter
Get Updates
Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.
Related Articles
Subscribe to:
Post Comments (Atom)






0 Responses to “MFAHAMU VIZURI MCHEZA BRIAN DEACON ALIYECHEZA FILAMU YA JESUS "YESU" MWAKA 1979 NA ANACHOKIFANYA SASA..!!”
Post a Comment
Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.