Tuesday, October 22, 2013

WANANCHI WAZUIA MSAFARA WA RAIS KIKWETE KWA MABANGO


Msafara wa JK ukiwa umezuiwa eneo la Mbwila Ludewa leo 
Wananchi wa Mlangali wakiwa wamezuia msafara wa Rais Kikwete 
Madai ya wana Ludewa kwa JK 
Msafara wa JK ukiwa umezuiwa eneo la Mbwila Ludewa leo 
Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe kushoto akisaidia 
kueleza kero za wana Ludewa kwa Rais Kikwete baada ya msafara wake 
kuzuiwa eneo la Mlangali leo 


mwandishi wa 
habari wa TBC Mbeya Bw Hosea Cheyo akiondoka eneo la tukio katika 
Hospital ya Ludewa baada ya maofisa usalama wa Kikwete kutimua 
wanahabari wasio kuwa na vitambulisho vya Ikulu jambo ambalo limepingwa
na wahabari kuwa ni unyanyasaji mkubwa 
MBUNGE wa jimbo la Ludewa 
Deo Filikunjombe awafyatua mawaziri mbele ya Rais Jakaya 
Kikwete kuwa wamekuwa wakitembelea jimbo lake la Ludewa
wakati wa ziara ya Rais na waziri mkuu wakati 
siku zote wananchi 
wa jimbo hilo 
wanalia kwa kero mbali mbali.
Mbali ya kuwawasha mawaziri hao pia 
mbunge Filikunjombe amesema kuwa kero ya maji katika mji wa Ludewa ni kubwa na wananchi kwa zaidi ya
wiki moja sasa hawana maji yamefungwa
kwa ajili ya kuelekea Ikulu kwa matumizi ya 
Rais hali wananchi wa mji huo
akiwemo yeye mwenyewe wamekosa maji ya kuoga kwa zaidi ya siku tatu sasa
Mbunge Filikunjombe alitoa
kauli hiyo leo katika uwanja wa Ludewa
wakati wa mkutano wa hadhara wa
Rais Kikwete.
Kwani alisema kuwa 
mbali ya jitihada mbali mbali ambazo serikali ya Kikwete imekuwa ikifanya katika kusukumba mbele
maendeleo ya wana Ludewa kwa kuanza
ujenzi wa lami , mradi mkubwa wa makaa ya mawe na mchuchuma ila 
bado wananchi hao hawana shaka na miradi hiyo isiyo kuwa wanataka miradi 
hiyo inanze kuwanufaisha wana Ludewa hata kwa ajira badara ya wageni kutoka Kenya kupewa vitalu katika
migodi hiyo huku 
wakazi wa Ludewa wakipokonywa vitalu vyao.

Hata hivyo alisema 
kuwa ni vema miradi hiyo kuanza kwa kuwanufaisha wana Ludewa
kwanza hata kwa ajira badala ya
kuwatazama wageni kutoka Kenya ambao wamekuwa 
wakipewa vitalu katika
miradi hiyo .
“Mheshimiwa Rais sisi Ludewa si kama Mtwara ambao 
walisema gesi haitatoka Mtwara ….sisi
Liganga na mawe yatatoka kwenda mikoa
mingine ila tunataka vijana wa Ludewa waanze kunufaika kwa ajira “

Pia 
mbunge huyo alisema kuwa
anashangazwa na baadhi ya mawaziri akiwemo 
waziri wa nishati ambae amekuwa akifikia 
wilaya ya Ludewa wakati wa ziara ya Rais badala ya kujenga utamaduni
wa kuwatembelea wananchi mara kwa mara.

Alisema wananchi wa Ludewa wamekuwa na kero
kubwa juu ya madini yao kwa wenyeji 
kupokonywa vitalu vyao na ofisi ya madini kanda nay eye kama mbunge
amepata kufika ofisi ya waziri husika ila hakuna jibu la maana analolitoa kwake .
Hivyo kumwomba Rais Kikwete 
kuwabana mawaziri hao ikiwezekana ofisi ya madini kujengwa Ludewa na sio Mbeya kama ilivyo sasa.

Awali naibu waziri wa maji Dr Binilith Mahenge alimweleza 
Rais Kikwete kuwa wizara imetenga bajeti kwa ajili ya kufikisha maji katika vijiji
mbali mbali vya wilaya ya Ludewa pamoja na eneo la mji wa Ludewa 

Huku 
kwa upande wake naibu waziri wa nishati na madini George Simbachawene alisema kuwa 
wizara yake itaendelea 
kuwahudumia wananchi wa Ludewa na
kuwaomba viongozi wa wilaya hiyo kuandaa ukumbi ili wataalam 
wake kuja kukutana na wananchi kwa ajili ya kupokea kero 
mbali mbali.

Wakati huo 
huo wananchi wa kata ya Madope na Mlangali 
katika wilaya ya Ludewa mkoani Njombe wamezuia 
msafara wa Rais Jakaya Kikwete kuomba 
kuharakisha ujenzi wa barabara ya lami 
kutoka Ludewa –Njombe pamoja na kero ya soko la mahindi
ambayo wamedai yameendelea kuharibika katika 
nyumba zao
Wananchi hao wakiwa na
mabango yanayoelezea kero hizo na nyingine walizuia msafara 
huo kwa nyakati tofauti wakati Rais Kikwete akitokea wilaya
ya Njombe kuelekea makao makuu ya wilaya ya Ludewa kwa ajili
ya ziara yake ya siku mbili wilayani Ludewa.
Kwa upande wao 
wananchi wa Madope ambako ni mpakani mwa wilaya ya 
Njombe na Ludewa walimwomba Rais Kikwete kusaidia kijiji 
hicho kupatiwa kituo cha afya pamoja 

na kuomba umeme , mnara wa
simu na barabara ya lami kutoka Njombe – Ludewa.
Wakati wananchi
wananchi wa kata ya Mlangali wakimwomba 
Rais Kikwete kuwasaidia masoko ya 
mazao yao pamoja na kupatiwa huduma ya maji.
Akijibu kero za wananchi hao Rais Kikwete
alisema kuwa serikali yake itaendelea 
kuwahudumia ikiwa ni pamoja na kutekeleza ahadi zake.
Alisema kuhusu suala la mazao
kukosa soko alisema kwa sasa serikali imenunua mazao kiasi cha 
kutosha na kuwa tayari imewataka watu binafsi kujitokeza kununua mazao 
hao.

Pia 
alisema suala la barabara tayari 
barabara ya Ludewa – Njombe ipo katika mkakati wa kujengwa kwa kiwango
cha lami na tayari ujenzi huo umeanza
katika mji wa Ludewa.
Kuhusu
suala la maji alisema kuwa kwa kawaida upo usemi usemao kuwa wageni 
njoo wenyeji tupone ila ameshangazwa kuona Ludewa ni tofauti wageni 
wanapokuja ndipo wananchi wanapata kero ya maji.
Ila mimi sikupenda ninapokuja ninyi mkose maji ....mimi nitaondoka 
kesho tu ila upo mkakati wa serikali wa kutatua kero ya maji mijini na
ninawaahidi katika kipindi kifupi kero hii ya maji itamalizika tayari 
bajeti ipo na shabaha yetu kutatua kero hiyo"
Akielezea
kuhusu suala la umeme alisema vijiji zaidi ya 74 vitanufaika na 
umeme vijijini vikiwemo vijiji vya Mlangali , Madope na vijiji 
vingine vyote vya njiani kuelekea Songea na tayari mkandarasi 
amepatikana na kuwataka wananchi kuanza mandalizi ya kuingiza umeme.
Hata 
hivyo Rais Kikwete akielezea kuhusu ujenzi wa barabara ya lami 
alisema kuwa kazi hiyo ina kazi zaidi ya moja ikiwemo ya uchoraji ramani
na upembuzi yakinifu zoezi ambalo linaendelea kabla ya zoezi la tatu 
kuanza.
Alisema 
kuwa kwa upande wa Ludewa tayari Km mbili na nusu zimekwisha jengwa 
na sasa wasubiri kuanza ujenzi wa barabara yote ya Ludewa - NJombe .
Kuhusu
ahadi ya meli ambayo mbunge Filikunjombe alimtaka Rais kutolea 
ufafanuzi alisema kuwa serikali ipo katika mchakato wa kutekeleza ahadi 
hiyo.
Alisema
kuwa serikali itanunua meli tatu kwa ajili ya maziwa matatu Tanganyika
, Nyasa na Victoria na kuwa tayari kupata meli zinafanyika na nchi 
zaidi ya mbili zinataka kuleta meli hivyo kuwa na meli mbili kila 
ziwa 

Rais
Kikwete alimtaka mbunge Filikunjombe kuendelea kufuatilia suala 
hilo kwa waziri DR Mwakyembe ili kuona ahadi hiyo inatekelezeka.

Credit: matukio daima

Tags:

0 Responses to “WANANCHI WAZUIA MSAFARA WA RAIS KIKWETE KWA MABANGO ”

Post a Comment

Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.

HHHHHHHHHHHH

Subscribe

Kwa habari na Taarifa weka Email yako Hapa tutakutumia

© 2014 FUNUNU HABARI.. All rights reserved.
Designed by FUNUNU HABARI